Jun 3, 2013

WIZARA YA HABARI KUISAIDIA TAASISI YA MUNIIRA MADRASA.
  • NI BAADA YA KURIDHISHWA NA UTENDAJI WAKE 
  • YAWAAGIZA WATENDAJI WAKE KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI BLOG YA MUNIRAMADRASA.

Serilkali ya mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kuisaidia taasisi ya Muniira Madrasa And Islamic Propagation Association ili  kufikia malengo yake yaliyojiwekea katika kutoa na kufikisha habari zilizo sahihi kwa jamii.

Ahadi hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki hii na waziri wa habari michezo,utamaduni na utalii wa Zanzibar Mheshimiwa Said Ally Mbrouk alipokua anazindua blog ya taasisi  hiyo katika viwanja vya muniira madrasa vilivyopo magomeni makuti jijini Dar es salaam.

Alisema wizara yangu imefurahishwa na juhudi za kisasa zinazotolewa na taasisi hii hasa kwa kutoa elimu kwa njia ya mtandao kwani ni njia ambazo zinazo hitajika katika  zama hizi.

Nanukuu"katika kuwaunga mkono hili,nawaagiza watendaji wangukuwapatia ushirikano mkubwa kwa kuwapatia habari na matukio yatokeayo kwa kuwa wao wanamtandao mpana katika ukusanyaji wa habari na waandishi mahiri akiwemo bwana Juma Mmanga ambae ana njia na uwezo mkubwa wa habari za ndani na nje za dini ya kiislam na za kijamii"mwisho wa kunukuu.

Alisema kwa kuanzisha chombo hicho cha habari kinatoa fursa pana ya kuwafikia watu wa sehemu mbalimbali na kuyafahamu mambo mbalimbali yanayojiri duniani.

Awali akisoma risala ya taasisi hiyo,katibu mkuu wa taasisi hiyo Al haj Juma Rashid alisema,taasisi hii inatoa elimu kwa njia kumi tofauti na njia mojawapo  miongoni mwa njia hizo kumi ni kutoa elimu na habari kwa njia ya ukurasa wa tovuti (blog) inayojulikana kwa anuani ya www.muniramadrasa.blogspot.com

Aidha alizitaja changamoto zinazo ikabili blog hiyo kuwa ni pamoja na uhaba wa kamera na kutokuwa na chombo cha usafiri,hii mbali ya kuwa ni kikwazo cha kufikia malengo yetu ya ujumla lakini pia itatukwaza kuyafikia matukio kwa wakati muafaka,alisema ustaadh juma.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu na masheikh mbalimbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi.


waziri wa habari,michezo,utamaduni na utalii wa zanzibar akizindua blog ya taasisi ya munira madrasa inayo julikana kwa jina la www.muniramdrasa.blogspot.com
kulia kwake ni afisa mnadhimu wa vyombo vya habari vya serilkali ya mapinduzi zanzibar ambaye pia ni amiri wa vyombo vya habari vya kiislam Tanzania maalim Juma Mmanga na kushoto kwake ni katibu wa taasisi Ustaadh Juma Rashid.Picha kwa hisani ya Said M.Bagenda.

Hapa waziri wa habari michezo,utamaduni na utalii wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar mheshimiwa sid ally mbaruok akiipitia blog ya taasisi ya munira madrsa muda mfupi baada ya kuizindua.picha kwa hisani ya Said M.Bagenda

0 comments:

Post a Comment