Jun 3, 2013

WAISLAMU WATOA TAMKO
  • NI KUHUSU KUSUDIO LA SERIKALI KUFUTA MITIHANI YA SOMO LA DINI MASHULENI.
  • WASEMA MAAMUZI HAYO YATAIATHIRI JAMII 
Hatimaye waislamu nchini Tanzania wametoa tamko la kupinga hatua zinazotaka kuchukuliwa na serikali ya kufuta mitihani ya taifa katika somo la dini hapa nchini.

Msimamo huo umetolewa jana na Sheikh Ponda  Issa ponda ambaye ni katibu wa kamati ya kutetea mali za waislamu nchini Tanzania.

Akitoa msimamo huo mbele ya waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Diamond jubilee,sheikh ponda alisema wana sababu nyingi na za msingi kupinga kusudio hilo la serikali huku akitaja ya kwamba waislamu hawakushirikishwa katika kufikia maamuzi hayo huku wakristo wakishirikishwa hatua kwa hatua.

Alisema sababu nyengine ni kwamba maamuzi hayo yataliathiri taifa kwa ujumla kwani kwa kufuta mitihani hiyo ina maanisha somo la dini mashuleni litakufa kibudu na kuwafanya watoto ambao ni sehemu ya jamii ya watanzania kukosa mafunzo ya kiroho na kusababisha kukithiri kwa kasi kubwa mmomonyoko wa maadili ambao kwa sasa unatishia silka na tamaduni ya watanzania.

Alidai wanazo taarifa kwamba serikali iliiagiza wizara ya elimu na ufundi ikae na wadau (waislamu na wakristo) ili kupata maoni yao lakini inaonekana wizara ya elimu na ufundi imehujumu agizo hilo na kuushirikisha upande mmoja pekee.

Aliendelea kudai kwa kuwaambia waandishi wa habari ya kwamba hata chombo cha Bakwata ambacho serikali inakitumia mara kwa mara wamesema  kwamba wao  (Bakwata) hawakushirikishwa zaidi ya kupewa taarifa baada ya kila kitu kukimaliza wao (wizara na taasisi za kikiristo)
.
Hii ni dhulma inayoambatana na dharau ya hali juu dhidi ya waislamu mabayo kamwe hatuwezi kukubali na tutaipinga kwa nguvu zetu zote,aliseama sheikh ponda.

Komngamano hilo lililoandaliwa na Baraza kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania lilihudhuriwa na waislamu wengi na kuufanya ukumbi utapike.

Hivi karibuni wizara ya elimu na ufundi  ilitangaza kusudio la kufuta mitihani kwa masomo ya dini  mashuleni.

Blog ya munira madrasa inaendelea na juhudi za kumpata msemaji wa wizara kuzungumzia msimamo huo wa waislam.

Sehemu ya waumini wa Dini ya kiislmu waliofurika katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Diomond jubilee kusikilza msimamo wa waislamu juu ya kufutwa kwa mitihani ya taifa katika smo la dini.
Picha na habari kwa hisani ya mwanahabari wetu Juma Rashid



Pichani Sheikh Issa Ponda akiwasilisha tamko la waislam kwa waandishi wa habari

0 comments:

Post a Comment