Mar 17, 2016

Mkutano wa kwanza wa Qur'ani wafunguliwa Senegal

Mkutano wa kwanza wa Qur'ani wafunguliwa Senegal
Mkutano wa kwanza wa Qur'ani huko magharibi mwa Afrika umefunguliwa nchini Senegal. 
 
Shirika la Habari za Qur'ani la IQNA limetangaza kuwa, Mkutano huo uliofunguliwa kwa anwani ya "Qur'ani Tukufu, Mwelekeo wa Kiroho na Ulimwengu Usio na Ukatili", ulifunguliwa jana mjini Dakar kwa hima ya Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Kaulimbiu kuu ya mkutano huo w siku mbili utakaomalizi leo ni udiplomasia wa Qur'ani kuelekea kwenye umoja wa Kiislamu. Mkutano huo unahudhiriwa na wataalamu na watafiti wa masuala ya Qur'ani wa Senegan na Iran. 

Pofesa Chernoka Habib ambaye ni mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Dakar amesema kuwa kufanyika mkutano huo ni miongoni mwa sababu za kuimarisha misingi ya umoja na mshikamano wa Kiislamu. 

Amesusitiza kuwa lengo la mkutano huo ni umoja na mshikamano baina ya Waislamu. 

Kwa upande wake Sheikh Abdul Muniin Zeun ambaye ni mjumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema dini ya Uislamu imejitenga kikamilifu na vitendo vya ukatili na utumiaji mabavu na kwamba Qur'ani tukufu imejuzisha tu harakati na mapambano ya kujihami, kuilinda nafsi, mali na matukufu ya watu.

0 comments:

Post a Comment