Mar 18, 2016

Mansour aswekwa rumande kwa tuhuma za kuchomwa kisonge


Wakati wananchi wa Tumbatu wakidai kuchoshwa na madhila wanayofanyiwa na vyombo vya ulinzi na kusababisha baadhi yao kuondoka kwenye nyumba zao kama alivyobainisha Bw. Chambu Ahmad Makame huku Mjini nako Jana jioni Mshauri wa Maalim Seif, Mansoor Yussuf Himid anashikiliwa na jeshi la polisi.

Kwa mara nyengine tena, Mansoor aliitwa na polisi jana kwa ajili ya mahojiano akiambatana na Wakili Karume Haji Mrisho ambaye amesema Mansoor ameshutumiwa kwa mambo mbali mbali ikiwemo suala la kuripuliwa Kisonge hata hivyo wamekataa kumpa dhamana hivyo ataendelea kuwepo polisi. Mwenyeenzi Mungu atuvushe na balaa katika nchi yetu

Orodha ya viongozi wa CUF wanaoshikiliwa na polisi Zanzibar kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu wa CUF Magdalena Sakaya, hadi sasa viongozi waliokamatwa ni pamoja na, Eddy Liamy mwanamikakati ya ushindi CUF; Nassoro Mazrui, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; Mahomoud Mahinda, Katibu Mtendaji JUVICUF; Abeid Hamis Bakari, Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi na Hamad Masoud, Mkurugenzi wa Habari CUF.

Tunatanguliza kuomba radhi kwa picha zinazofuata hapa chini.

chanzo:mzalendo net
 10320351_10206084593690652_3914197052680880597_n


1661062_10206084665532448_979295854373902536_n

999421_10206080035696705_2607240507663598007_n

10436012_10206076406725983_2853634443845755094_n

0 comments:

Post a Comment