Mar 18, 2016

Kaka wa mkuu wa al-Qaida aachiwa huru nchini Misri

Kaka wa mkuu wa al-Qaida aachiwa huru nchini Misri
Serikali ya Misri imetangaza kumuachilia huru kaka wa kiongozi mkuu wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaidah kutoka jela alikokuwa anashikiliwa.

Muhammad al-Zawahiri, kaka wa Ayman al-Zawahiri, ameachiliwa huru na mahakama ya jinai ya nchi hiyo. Hata hivyo kwa mujibu wa mahakama hiyo, kaka wa kiongozi mkuu wa genge hilo la kitakfiri atatakiwa kuripoti polisi kila siku. 

Muhammad al-Zawahiri, alitiwa mbaroni na polisi wa Misri, tarehe 17 mwezi Agosti mwaka 2013 wakati alipokuwa amejificha katikati ya wafuasi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin katika medani ya Rābia al-Adawiyya na al-Nahdha. 

Kabla ya hapo pia Muhammad al-Zawahiri alikuwa ameachiliwa huru na baraza la kijeshi la nchi hiyo mwaka 2011, hata hivyo alitiwa mbaroni tena baada ya kuondolewa madarakani Muhammad Mursi, rais wa zamani wa Misri ambaye hadi sasa anaendelea kushikiliwa na watawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment