Feb 21, 2015

TUSHINDANE KWA HOJA KUINUSURU NCHI YETU



Watanzania wametakiwa kushindana kwa hoja za msingi ili kulinusuru taifa la tanzania ambalo lipo njia panda.

Nasaha hizo zimetolewa jioni hii na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha Wananchi (CUF) Mhe Abdul Kambaya.

Mhe kambaya ameyasema hayo katika Mkutano Maalumu wa kuwapongeza Wananchi kwa kukiwezesha chama cha CUF kushinda mitaa mitatu kati ya mitaa sita ya kata ya Makumbusho,Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni,Dar es salaam.

Amesema,"Ndugu wa Tanzania,kwa mwenye akili timamu hashindani kwa sababu ana sauti kubwa,au ana mwili mkubwa,bali mwenye akili timamu anashindana kwa hoja za msingi".

Aliendelea kusema kwamba,Nchi yetu inakabiliwa na matatizo ya msingi,ambayo kuyataua kwake kunahitajika kupata chama makini na kiongozi makini,mwenye uwezo na uadilifu.

"Sisi wana CUFtunaposema tunamuunga mkono Profesa Ibrahimu Lipumba,si kwa sababu ya urefu wake,bali ni kwa sababu ya elimu na uwezo wake wa kuongoza" ,alisema.

Aliendelea kusema kwamba "Tanzania ina Maprofesa wengi,lakini wazungu wamemtangaza Profesa Lipumba kuwa ni Full Brighte kutokana na uwezo wake,na wanatushangaa kutuona hatumtumia vizuri".

"Nawasihi wananchi,kwa kua Mungu ametupa hekima,basi tuoneshe hekima kwa kufanya maamuzi sahihi,na hekima ni kukiweka kitu husika mahala pake,na utakapokiweka kitu husika mahala si pake utahesabika kua na mapungufu ya kufikiri" ,mwisho wa kumnukuu.

Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Bonde uliopo Mwanyamala Kisiwani.
Baadhi ya wapenzi na wanachama wa CUF wakifuatilia Mkutano huo.
Mhe Abdul Kambaya,akimtambullisha Kala Pina ambaye ni msanii wa kizazi kipya

0 comments:

Post a Comment