Sep 21, 2014

Zarif: Undumakuwili umepelekea ugaidi kuongezeka

Mohammad Javad Zarif Mohammad Javad Zarif
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, undumakuwili na sera zisizo sahihi ndizo sababu kuu za kuimarika makundi ya kigaidi yenye misimamo mikali katika eneo la Mashariki ya Kati.
Mohammad Javad Zarif ameyasema hayo mjini New York katika mkutano na mwenzake wa Australia Julie Bishop.

 Zarif ameongeza kuwa kunahitajika juhudi za pamoja na sera mpya kukabiliana na uovu wa ugaidi. 

Zarif ameendelea kusema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipatia uzito mkubwa suala la kuisaidia nchi jirani ya Iraq kuimarisha usalama wake.

Wakati huo huo Zarif amesema Iran haitashirikiana na Marekani kupambana na kundi la kigaidi la Daesh (ISIL). 

Ameongeza kuwa, Tehran imekataa pendekezo hilo kutokana na kutokinaika kwamba serikali ya Marekani ina nia hasa ya kupambana na kundi la kigaidi la Daesh.

0 comments:

Post a Comment