Sep 4, 2014

UN: Israel imewaacha Wapalestina wengi bila makao

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa, zaidi ya Wapalestina laki moja hawana makao kutokana na mashambulizi ya siku 50 ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Ripoti hiyo inasema nyumba nyingi za Wapalestina ama zimeharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutumika tena au zimebomolewa kabisa. 

Umoja wa Mataifa aidha umesema zaidi ya Wapalestina 60 000 wanaishi katika shule za Umoja wa Mataifa jambo linalokwamisha masomo katika Ukanda wa Gaza. 

Ripoti ya UN umetolewa huku makundi ya kutetea haki za binadamu ndani na je ya Palestina yamesema kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa, utawala haramu wa Israel ulitumia mabomu yaliyopigwa marufuku kimataifa kwenye mashambulizi yake ya kinyama ya siku 50 huko Gaza. 

Zaidi ya Wapalestina 2000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto waliuawa shahidi kwenye hujuma hiyo. 

Wengine zaidi ya 11000 walijeruhiwa.

0 comments:

Post a Comment