Aug 7, 2014

Wakristu watoroka Qaraqosh Iraq

Bendera ya wapiganaji wa Isis walioteka mji wa Qaraqosh ikipepea Mosul

Maelfu ya Wakristu wanatorokea maisha yao katika mkoa wa Nineva baada ya wapiganaji wakiislamu wa
The Islamic State kuuteka mji wa Qaraqosh.

Afisa wa ngazi ya juu wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq ameonya kuwa watu 50,000 wa jamii ya Yazidi watakabiliwa na njaa ikiwa hawatapata msaada wa dharura.

Jamii ya Yazidi ilikimbilia maeneo ya milima ikiwa na chakula kidogo na maji baada ya wapiganaji wa jihad kutoka kwa kundi la Islamic State kuvamia mji wa Sinjar mwishoni mwa wiki.
Wapiganaji wa Kikurdi Peshmerga awali wakidhidbiti mji huo wa Mosul.

Jabbar Yawar, ambaye ni kiongonzi wa wapiganaji wa kikurdi anasema kuwa tayari wengi wao wameaga dunia
Kutekwa kwa mji wa Qaraqosh kumesababisha kukimbia kwa maelfu ya watu kaskazini mwa Iraq kutokana na vitishovya makundi ya Jihad.

Kushindwa kwa vikosi vya kikurdi kudhibiti mji huo na mji mingine kutoka kwa mikono ya wapiganaji wa Islamic State kutasabaisha mengi..

Wapiganaji wa Kikurdi wa Peshmerga walikimbia mji huo bila kupingwa.
Kasisi mmoja mkuu wa eneo hilo ameliambia shirika la Habari la Ufaransa kuwa, maelfu ya watu wanaonekana wakikimbia kwa hofu.
Jamii ya Yazidi ikitoroka mji huo
Kuondoka kwa watu hao kunafutia kuondoka kwa wakrito wengine kutoka mji wa Mosul baada ya kuamrishwa kundoka , kubadili dini au kuawa na wapiganaji wa Jihad.

wapiganaji wa The Islamic State wameteka kiasi kikubwa tu cha ardhi kutoka Iraq na Syria ambayo wametangaza kuwa taifa la kiislamu.

Inakisiwa kuwa wakaazi laki moja wameshatorokea maeneo ya Kurdistan.

0 comments:

Post a Comment