Aug 14, 2014

Libya: mkuu wa polisi wa mji wa Tripoli auawa

Mapigano yaendelea kurindima kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli.
Mapigano yaendelea kurindima kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli.

Maafisa wa usalama nchini Libya wamethibitisha kuuawa kwa mkuu wa polisi wa mjini Tripoli, Kanali Mohamed al-Suissi, na watu wasiojulikana katika kitongoji cha mji mkuu mashariki mwa Libya.

Msemaji wa polisi nchini Libya ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa kanali Suissi ameuawa na kundi la watu wasiojulikana waliokuwa na silaha ambapo watu wawili waliokuwa pamoja naye wametekwa nyara.

Shirika la habari la taifa hilo Lana, limethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kwamba uchunguzi umeanzishwa kubaini waliotekeleza mauaji hayo.

Viondozi wa mpito wa Libya wameshindwa kurejesha hali ya utulivu nchini tangu kuangushwa kwa utawala wa Mouammar Kadhafi katika mwaka 2011.

Mauaji ya mkuu wa polisi katika mji wa Tripoli, yanatokea kukiwa na mapigano kati ya makundi ya wanamgambo hasimu kuhusu umiliki wa uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Kwa mujibu wa viongozi, watu 124 wameuawa katika machafuko hayo, watu wengine 500 wamejeruhiwa, huku watu 36.000 wameyahama makaazi yao.

0 comments:

Post a Comment