Aug 14, 2014

BAMAKITA wampongeza Mwigulu,

BARAZA la Maadili la Kiislamu nchini (BAMAKITA), limeunga mkono kauli iliyotolewa na Mbunge wa Iramba Magharibi, mkoani Singida, Bw. Mwingulu Nchemba kutaka vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, viahirishwe ili kuokoa fedha za walipakodi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa baraza hilo, Shekhe Athuman Mkambaku, alisema kauli ya Bw. Nchemba inaonesha ni mzalendo halisi anayelipenda Taifa lake.

Alisema hivi karibuni, Bw. Nchemba alishauri Bunge hilo liahirishwe kwani wajumbe waliopo hawawezi kuwapatia Watanzania Katiba Mpya kutokana na theluthi mbili inayotakiwa kwa mujibu wa sheria, haiwezi kupatikana kwa sababu baadhi ya wajumbe kutoka upinzani hawashiriki vikao vya Bunge hilo.

"Kuendelea kuwalipa posho wajumbe wa bunge hili ni matumizi mabaya ya fedha za umma...Nchemba ameonesha ukomavu wa kisiasa na maneno yake hayapaswi kupingwa wala kupuuzwa bali aungwe mkono na kupongezwa," alisema.

0 comments:

Post a Comment