Jul 4, 2014

Wanajeshi na polisi wa Misri wawaua watu 17 wenye siasa kali

Ofisa wa idara ya usalama ya Misri amesema wanajeshi na polisi wa Misri wamewaua watu 17 wenye siasa kali mjini Rafah mkoa wa Sinai Kaskazini. 

Ofisa huyo amesema watu 12 wenye siasa kali walikuwa kwenye magari manne na kupita karibu na mji wa Rafah, na wanajeshi na polisi wa Misri waliwashambulia kwa kutumia vifaru na kuwaua watu wote. Inasemekana kuwa watu hao ni wanachama wa kundi la "Ansar Bayt al-Maqdis".
Watu wengine wanane wenye siasa kali walijaribu kuweka mabomu mjini Rafah, na wanajeshi na polisi wa Misri waliwagundua na kuwaua watano kati yao, na kuwakamata wengine watatu. 

Jana ulitimia mwaka mmoja tangu rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondolewe madarakani. Waungaji mkono wa Bw. Morsi na kundi la Muslim Brotherhood walifanya maandamano ya kuipinga serikali katika sehemu nyingi, na kupambana na polisi. 

Aidha, matukio zaidi ya kumi ya milipuko ya mabomu yalitokea katika sehemu mbalimbali nchini Misri na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watano.

0 comments:

Post a Comment