Apr 23, 2014

Waislam wahamishwa Bangui ili kunusuru maisha yao

Zaidi ya waumini 100 wa kiislamu wamehamishwa na wanajeshi wa kikosi cha Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika Kati toka mji mkuu Bangui na kupelekwa katika eneo linalodhibitiwa na waasi wa zamani wa Seleka.

Machafuko katika Jamhuri ya Afrika Kati
Maafisa wa Umoja wa mataifa wanasema waumini hao wa kiislam wamehamishiwa Bambari umbali wa kilomita 300 toka mji mkuu Bangui ili kuepukana na matumizi ya nguvu na visa vyenginevyo vya kikatili. 

Mlolongo wa magari yaliyokuwa yakiwahamisha uliongozwa na vikosi vya wanajeshi wa Ufaransa wanaotumikia opereshini Sangaris,shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa linalowashughulikia wahamiaji.

"Ni opereshini ya kuokoa maisha iliyoanzishwa kama hatua ya mwisho baada ya kutafakari kwa muda mrefu" amesema Tammi Sharpe ambae ni msaidizi wa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi katika Jamhuri ya Afrika Kati.

Watu hao waliokuwa wakiishi katika mtaa wa kaskazini wa PK 12,walikokuwa wakiishi watu wa imani tofauti hapo awali,wamekuwa wakihujumujiwa kila mara na kugeuka mhanga wa visa vya kila aina vya ukandamizaji .

Walikuwa wakiishi katika hali ngumu kupita kiasi".Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema.

Waumini wengi wa kiislam wanaoishi katika mtaa huo huo watahamishwa pia ikiwa wenyewe wataridhia na viongozi wa serikali ya mpito wataruhusu-amesema bibi Tammi Sharpe.

Mlolongo wa magari watupiwa mawe
Wapiganaji wa kikristo Anti Balaka
Mlolongo wa magari yaliyokuwa yakiwasafirisha waislam hao uliotupiwa mawe huko Sibut,kilomita 200 kutoka Bangui, eneo linalodhibitiwa na wanajeshi wa kulinda amani wa kutoka nchi za Afrika MISCA.

Wengi wa waumini wa dini ya kiislam walilazimika kuuhama mji mkuu Bangi tangu waasi wa Seleka -chanzo cha mapinduzi ya machi 2013,walipolazimika kuikabidhi uongozi serikali ya kiraia januari mwaka huu.

Tangu wakati huo Umoja wa mataifa umekuwa ukizungumzia juu ya takasa takasa ya kikabila inayofanywa na wanamgambo wa kikristo wa Anti Balaka.

Mapigano yanaendelea
Maafa yanayowakumba binaadam katika jamhuri ya Afrika kati

Kwa mujibu wa meya wa Bambari, El Haj Abacar ben Ousmane, wakaazi 45 elfu,wa mji huo wakristo na waislamu wanaishi kwa amani tangu zamani.

"Hatuna tatizo la kuwakaribisha wengine.Kwetu sisi watu wote ni sawa."Amesema.

Wakati huo huo mapigano yameripotiwa kati ya wanamgambo wa kikristo na wanajeshi wa Ufaransa katika mji wa kati wa Grimari.

Watu kadhaa wanasemekana wameuwawa.

Msemaji wa vikosi vya Ufaransa katika eneo hilo Sebastien Isern amesema wanajeshi wao walishambuliwa na wanamgambo wa kikristo Anti Balaka walipotaka kuzuwia mapigano kati ya wanamgambo hao na wale wa kiislam wa Seleka.

0 comments:

Post a Comment