Mtoto Satrine akiwa amepakatwa na babake.
Madaktari
katika hospitali kubwa zaidi ya umma nchini Kenya,Kenyatta,
wamefanikiwa kutoa risasi iliyokuwa imekwama katika ubongo wa mtoto
Satrine Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Risasi hiyo iliyomuingia mtoto Satrine kichwani ndiyo iliyomuua mamake.
Mamake Satrine alikuwa amempakata mtoto
wake ili kumlinda kutokana na magaidi waliovamia kanisa walimokuwa wiki
moja iliyopita katika mtaa wa Likoni mjini Mombasa.
Lakini
walimpiga risasi mama huyo na kumuua papo hapo huku risasi iliyomuua
mama huyo ikiingia kichwani mwa Satrine na kukwama kwenye ubongo wake.
Satrine
alipelekwa Nairobi kwa matibabu maalum kutoka Mombasa kutokana na
ukosefu wa wataalamu wa upasuaji wa ubongo mjini humo.
Shughuli
ya kuondoa risasi hiyo ilichukua saa tatu na ilifanywa na madaktari
watatu wakiongozwa Daktari Mwangi Gichuru ambaye ni mkuu wa kitengo cha
upasuaji wa neva katika hospitali hiyo.
Matoto Satrine yuko salama na daktari Mwangi anasema hawakupata matatizo walipokuwa wanafanya upasuaji huo
Apr 2, 2014
MADAKTARI WAFANIKIWA KUITOA RISASI KATIKA UBONGO WA MTOTO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment