Mar 2, 2014

WADAU WA ELIMU YA KIISLAMU WAKUTANA KUANZISHA BODI YA ELIMU


BAADHI YA VIONGOZI WA BARAZA KUU WAKIWA PAMOJA NA VIONGOZI WA TAMPRO KATIKA MKUTANO HUO.
Wadau wa elimu ya kiiislamu nchini leo wamekutana kwa dhamira ya kuanzisha bodi ya elimu ya Wiislamu nchini Tanzania.

Wadau hao wamekutana leo hii katika ukumbi wa Lamada Uliopo Ilala Jijini  Dar es salaam.


Akiongea na mwandishi wa munira blog,katibu mkuu wa TAMRO Doctor Pazi Mwinyimvua amesema Waislamu kuwa nyuma katika sekta ya elimu kuna tokana na Historia iliyopo,kwani Wazungu walipokuja waliwanyima elimu Waislamu na hata ikalazimika baadhi ya Waislamu kubadili majina au kuingia katika ukafiri ili wapate elimu.

"lakini hata tulipo pata uhuru Serikali ilifanya juhudi ya kuyapa kipaumbele makundi maalum ikiwemo wafugaji,akina mama na wengineo lakini bado juhudi hizo hazijaleta natija mzuri kwa waislamu".

"Huu si wakati wa kuendelea kulaumu,bali ni wakati wa kujipanga na njia moja wapo ya kujipanga ni sisi wadau wa elimu tujiunge pamoja,bila shaka tukiwa na bodi ya elimu ya waislamu,itatusaidia",mwisho wa kumnukuu. 

Mkutatano huo uliowajumuisha wadau wa elimu ya kiislamu umeandaliwa na baraza kuu la jumuiya na taasisi za kiislamu kwa kushirikiana na TAMRO.

Hadi mwandishi wetu anaondoka,mkutano bado unaendelea.
 
 USTAADH JUMANNE MPINGA AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA MUDA WA MCHAKATO WA KUANDAA MKUTANO WA WADAU WAELIMU AKIWASILISHA MADA YA UMUHIMU WA KUWA NA BODI YA ELIMU YA WAISLAMU NCHINI TANZANIA.
BAADHI YA WADAU WAKIFUATILIA YANAYO WASILISHWA KATIKA MKUTANO.


MDAU WA ELIMU KUTOKA UNUNIO BAGAMOYO,AKICHANGOA MADA

0 comments:

Post a Comment