Mar 28, 2014

MVUA ZAANZA KULETA MAAFA DAR

Neema ya mvua zinazo endelea kunyesha jijini Dar es salaam,zimeanza kuleta maafa.

kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Munira blog umegundua kwamba watu kadhaa wameathirika na mvua hiyo.

Munira blog ilishuhudia kuta za nyumba kadhaa maeneo ya Mbagala Zakhem na Mbagala Kingugi zikiwa zimevunjika kutokana na mvua zilizo nyesha usiku wa kuamkia jana.

Aidha Munira Blog pia imeshuhudia maji kufurika katika Mto wa Ng'ombe unaokatiza maeneo ya Mwananyamala Kisiwani huku vitu mbalimbali vikonekana kuelea.


Nao wakaazi wamabondeni wamekuwa katika wakati mgumu baada ya maji kuingia katika nyumba zao.

Hayo yameshuhudiwa na mwandishi wetu Asubuhi hii alipofika maeneo ya Jangwani na kukuta Mto wote umemezwa na maji yanayokaribia kufunika barabara.

kwa upande mwingine mvua hizo zimewarahisishia wanaofanya biashara ya kuokota chupa za plasitiki baada ya chupa hizo kuelea na kutuwama kwa wingi maeneo ya jangwani kama walivyokutwa na mwandishi wetu hivi punde.

0 comments:

Post a Comment