Feb 21, 2014

Rouhani: Waislamu wakiungana wataikomboa Palestina



Salim Zanuon (kushoto) na Rais Rouhani Salim Zanuon (kushoto) na Rais Rouhani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa iwapo watu wa Palestina na Waislamu wa mataifa yote duniani wataungana na kuwa kitu kimoja basi wataweza kuzikomboa ardhi za Palestina ambazo zimevamiwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran alipokutana na kufanya mazungumzo na Salim Zanuon Spika wa Bunge la Palestina.
Katika kikao hicho Rouhani ameongeza kuwa kukombolewa Quds Tukufu ni tarajio la taifa la Iran na kwamba taifa la Palestina lina nafasi maalumu miongoni mwa Wairani. 

Rais Rouhani amesema mifarakano miongoni mwa Wapalestina ni kwa maslahi ya Israel na kuongeza kuwa nchi za Kiislamu zinapaswa kukurubisha mitazamo yao kuhusu mustakbali wa Palestina ili kadhia hiyo itatuliwe haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake Salim Zanoun amesema Wapalestina wanafahamu namna Iran ilivyowasaidia kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na nchi zingine. 

Ameelezea matumaini yake kuwa ulimwengu wa Kiislamu utaweza kutatua kadhia ya Palestina. Zanoun ameendelea kusema, hivi sasa Israel inatekeleza njama za kuiangamiza Quds Tukufu na kwa msingi huo ametoa wito kwa Iran kuchukua hatua zaidi za kuzuia njama hizo zilizo kinyume cha sheria.

0 comments:

Post a Comment