Feb 14, 2014

Rais mpya wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ajianda kukabiliana na kundi la wakristo la anti-balaka

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, februari 5 mwaka 2014 mjini Bangui
Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, februari 5 mwaka 2014 mjini Bangui

Rais wa jamhuri ya Afrika ya kati Catherine Samba-Panza na Jean-Yves Le Drian waziri wa ulinzi wa Ufaransa wametembelea katika mji wa Mbaiki uliopo kwenye umbali wa kilometa 80 kusini magharibi mwa jiji la Bangui.
Viongozi hao wote kwa pamoja wametowa ujumbe mzito kwa makundi yote ambayo bado yanashikilia silaha na ambayo yanaendesha mauaji hususan kundi la wanamgambo wa kikristo wa anti-balaka.

Catherine Samba-Panza amewataka wananchi wa taifa hilo kuridhiana na kueshi kwa pamoja kama zamani, huku akivitaka vyombo vya habari vya kimataifa kuyazungumzia mambo yalio chanya pia na kutozamilia pekee kwenye mambo yalio hasi.

Kuhusu swala la kuligawa taifa hilo sehemu mbili ambalo moja utakuwa ni upande wa wakristo na mwingine wa waislamu, ambalo limekuwa likizungumziwa sana nchini humo, waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amesema hakuna mpango huo na hakuna ataye kubali swala hilo.

Rais Panza ameahidi vita dhidi ya wanamgambo wa anti-balaka iwapo wataendeleza mauaji na kwamba wasifkiri kwa vile yeye ni mwanamke hawezi lolote, na iwapo watarudi tena kutekeleza mauaji ndio watatambua kuwa ni mwanamke kweli hawezi au la.

0 comments:

Post a Comment