Feb 13, 2014

Majeshi ya kimataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati huenda yakatumia nguvu iwapo mauaji yataendelea

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian wakati akuzuru majeshi ya Ufaransa nchini Mali
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian wakati akuzuru majeshi ya Ufaransa nchini Mali

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amesema kwamba vikosi vya Jumuiya kimataifa vipo tayari kusitisha vurugu za kidini zinazoendelea nchini jamhuri ya Afrika ya kati kwa kutimia nguvu iwapo itahitajika. Kundi la Anti Balaka, linaonekana kuwa kikwazo kwa amani ya Jamhuri ya Afrika ya kati

Wakati huo huo shirika la Amnesty International limewatolea wito wadau wa kimataifa kuhusu mauaji ya kikabila yanayo tekelezwa dhidi ya waumini wa Kiislam magharibi mwa nchi hiyo huku vikosi vya Jumuiya ya kimataifa vikiwa havija faanikisha kukomesha machafuko hayo.

Waziri wa ulinzi amesema inabidi makundi yote ya waasi wakomeshe mauaji la sivyo amevitaka vikosi vya kimataifa kutumia azimio la Umoja wa Mataifa linalo ruhusu kutumia nguvu iwapo itahitajika.

Kauli hii ya waziri wa Ulinzi wa Ufaransa inakuja baada ya ile ya viongozi wa kijehi wa Ufaransa na wa Umoja wa Afrika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati misca wakitishia kuwachukulia hatuwa kali waasi wa kikristo wa anti-Balaka wanaoonekana kwa sasa kuwa kikwazo cha kupatikana kwa amani nchini humo.

Waziri Le Drian anasubiriwa leo jijini Bangui ambapo anazuru nchi hiyo kwa mara ya tatu tangu kuanza kwa operseheni Sangaris mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana. 

Jijini Bangui waziri huyo wa ulinzi wa Ufaransa atakutana na rais wa nchi hiyo Catherine Samba-Panza.

0 comments:

Post a Comment