Feb 21, 2014

Huenda UN ikatuma majeshi yake CAR

Maombolezo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, anasema polisi na wanajeshi 3000 zaidi wanahitajika katika Jamhuri ya Afrika ya kati kuwalinda raia dhidi ya ghasia zinazoendelea.

Maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Afrika wapo nchini humo katika jitihada za kusitisha mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa kiislamu,Seleka na wapiganaji wa Kikristo wajulikanao kama Anti-Balaka.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yake ya siku tatu, maritibu wa misaada wa Umoja huo wa mataifa, Valerie Amos, amesema ameshtushwa na kiwango cha ukosefu wa usalama.

Mwandishi wa BBC katika Umoja wa Mataifa anasema kuna uwezekano mkubwa kwamba Umoja huo utawatuma wanajeshi wake wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini hilo huenda likachukuwa miezi kadhaa na hatua za dharura zinahitajika ili kuthibiti ghasia zinazoenea.

0 comments:

Post a Comment