Feb 25, 2014

UISLAMU SI UGAID-DOCTOR MAHMOUD


BAADHI YA WASHIRIKI WA KONGAMANO LILILOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI KATIKA MSIKITI WA KICHANGANI.


Jamii ya kitaifa na kimataifa imetakiwa kuelewa kwamba Uislamu si ugaidi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa kituo cha kiislam cha kimisri nchini Tanzania Dokta Sheikh Osama Mahammoud.


Dokta Osama ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kungamano la lililofanyika katika msikiti wa Michangani Jijini dar es salaam.

Amesema kuwa na kelele duniani juu ya machafuko mbalimbali kuhusishwa na Uislamu kitu ambacho si sahihi.

Amesema "Uislamu mbali ya kupinga msimamo mkali lakini pia unapinga mauwaji yasiyo na hatia,hivyo ukimuona mtu anaua au watu wanaua pasipo hatia basi hao wanafanya kwa utashi wao tu na si msimamo au mafundisho ya Uislamu"

"Mtume Muhammad S.A.W amesema wahurumieni walioko ardhini nanyi mutahurumiwa na walioko mbinguni,hii ni ishara tosha kwamba uislamu unataka tuishi kwa amani na ndiyo tafsiri sahihi ya neno UISLAMU"Mwisho wa kumnukuu.

kongamano hilo la siku moja liliandaliwa kwa ushirikiano wa kituo cha Kiislam cha Kimisri nchini Tanzania kwa kushirikiana na uongozi wa Msikiti wa Kichangani.

0 comments:

Post a Comment