PICHANI;WANAFUNZI WA MADRASA WAKIFANYA MITIHANI,MWAKA JANA
Jumla ya wanafunzi 1450 wa madrasa mbalimbali zilizopo katika mkoa wa Dar es salaam,kesho In Shaa Allah,watafanya mitihani ya pamoja.
Mitihani hiyo itakayoanza saa mbili Asubuhi itafanyika katika Shule ya Yemen iliyopo Chang'ombe Jijini Dar es salaam.
Akiongea na Munira blog,katibu mkuu wa Idara ya Madrasa DYCCC Sheikh Ramadhan Kwangaya,amesema "maandalizi yamekwenda vizuri, tunasubiri saa ifike wanafunzi wafanye mitihani"
Aliendelea kusema "tunataraji kushuhudia ushindani wa hali ya juu kutoka kwa wanafunzi,kwani baada ya ukaguzi tumegundua wanafunzi wamejiimarisha zaidi".
Kwa mujibu wa ratiba hiyo mitihani hiyo itaanza saa mbili asubuhi na kumalizika saa kumi jioni ambapo jumla ya masomo kumi yatafanyiwa mitihani.
Mitihani hiyo ni maalumu kwa madrasa ambazo zinatumia mtaala wa DYCCC ambapo Munira Madrasa ni moja kati ya madrasa zitakazoshiriki mitihani hiyo.
0 comments:
Post a Comment