Jan 10, 2014

WALIOUNGULIWA NA MOTO NYUMBA ZAO PEMBA,WAPATA MISAADA.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud akiwakabidhi Nguo na Vifaa vwengine Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Pemba baada ya kuunguliwa na moto nyumba zao hivi karibuni na kulazimisha zaidi ya Familia kumi na tano kukosa mahali pa kukaa baada ya nyumba zao kuungua moto.Akikabidhi viafaa hivyo kwa wananchi hao huko micheweni   

BAADHI ya wananchi wa shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba, wakielekea kwenye makaazi yao, mara baada ya kukabidhiwa msaada wa magodoro na vifaa vyengine, na waziri wa nchi afisi ya Makamu wa pili Mh: Mohamed Aboud Mohamed kwa niaba ya rais wa Zanzibar.


WANANCHI waliounguliwa moto nyumba zao hivi karibuni, shehi za shumba mjini na Maziwang’ombe wilaya ya Micheweni, wakitafakari jinsi ya kusafirisha msaada wa vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja na magodoro, waliokabidhiwa na waziri wa nchi afisi ya Makamu wa pili Mh: Mohamed Aboud Mohamed, kwa niaba ya rais wa Zanzibar

0 comments:

Post a Comment