Jaji wa mahkama hiyo Fatma Hamid Mahmoud ametoa ombi hilo alipokuwa akiendesha kesi inayowakabili viongozi hao katika mahakam kuu vuga mjini Zanzibar .
Jaji huyo pia ameutaka upande wa mashtaka kuwasilisha kwa maandishi sababu za kuzuiya dhamana ya viongozi hao waliokaa rumande kwa mwaka mmoja sasa.
Hatua hiyo imekuja baada ya mwendesha mashtaka wa Serikali Rashid Abdalla kudai kuwa vielelezo vya ushahidi wa kesi hiyo tayari vimekamilia hivyo ipangiwe tarehe nyengine ili kuwasilisha vielelezo vya mashahidi.
Kwa upande wake wakili anaesimamia watuhumiwa wa kesi hiyo Abdalla Juma ameiomba mahkama kupanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo na vielelezo viwasilishwe mahkamani hapo kutokana na ushahidi wa kesi hiyo kukamilika.
Hata hivyo upande wa mashitaka haukuwa na pingamizi na na ombi hilo na umedai kuwa unaiachia mahkama kuamua.
Watuhumiwa katika kesi hiyo ni Amiri mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Samahatu Sheikh Farid Hadi Ahmed mkaazi wa mbuyuni,Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kiislam Zanzibar Fadhilatu Sheikh Mselem Ali Mselem mkaazi wa kwa mtipura, Ustaddh Mussa Juma Mussa mkaazi wa makadara
Wengine ni Maustadh Suleiman Juma Suleiman mkaazi wa makadara, Khamis Ali Suleiman mkaazi wa mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma mkaazi wa Mwanakwerekwe ,katibu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislam Zanzibar Abdallah Said mkaazi wa Misufini na Fikirini Majaliwa Fikirini.
Mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali, uchochezi,ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa.
Kosa la nne linamkabili mshitakiwa namba nne al-. naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam Zanzibar Ustadh Azan Khalid ( mkaazi wa mfenesini.
Ustadh Azan Khalid Hamdan anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Jaji Fatma ameikhirisha kesi hiyo na kutaka upande wa mashitaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya kesi hiyo kabla ya januar 31 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment