Jan 4, 2014

Mahmoud Abbas kuushitaki utawala wa Kizayuni

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ametishia kuchukua hatua za kisheria na kidiplomasia dhidi ya Israel kutokana na kujenga kinyume cha sheria vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina. 

Akizungumza huko mjini Ramallah katika Ukingo wa Magharibi kwa mnasaba wa kutimia miaka 49 ya kuasisiwa harakati ya Fat-h Abbas amesema, Palestina itatumia haki yake kama mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Mataifa kuhitimisha siasa za Israel za kupenda kujitanua katika ardhi za Palestina.
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza kuwa, hawatoendelea kukaa kimya huku vitongoji hivyo ambavyo ni kama saratani vikizidi kusambaa hasa katika mji wa Quds.

Israel inaendeleza siasa za kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina ili kuzuia kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Baitul Muqaddas. 

Hii ni katika hali ambayo vitongoji hivyo si halali kwa mujibu wa maazimio mengi ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

0 comments:

Post a Comment