Jan 21, 2014

AKINA MAMA,MUNAYO FURSA YA KUSOMA ZAIDI;NASAHA



UKHT THUWAIBA NURDIIN HUSSEIN MUDA MFUPI BAADA YA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UZAMILI UONGOZI NA UTAWALA YA CHUO KIKUU CHA MZUMBE,

Wanawake wa Kiislamu wametakiwa kujituma zaidi katika safari ya kutafuta elimu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Nasaha hizo zimetolewa hivi karibuni na Ukht Thuwaiba Nurdin Hussein ambaye alitunukiwa Shahada ya Uzamili Uongozi na Utawala Chuo Kikuu Mzumbe.
Akiongea na Munira Blog Ukht Thuwaiba (ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria) amesema "kwa hakika Biidhni LLAAH hakuna kinachoshindikana,muhimu ni kuwa na nia ya dhati na kisha nia hiyo iambatane na juhudi za makusudi huku ukiweka mbele kumtegemea ALLAH"

Aliendelea kufafanua ya kuwa "mimi ni mfanyakazi lakini nilikuwa najisomea jioni baada ya saa za kazi,hatimaye nimefanikiwa kupata shahada hii".

"Bado nina nia ya kujiendeleza zaidi kielimu,kwani kutafuta elimu ni Amri ya ALLAH,nami nawajibika kuitii amri hiyo ili nipate radhi za allah".

Ukht Thuwaiba alisema wanawake wa kiislamu wanayofursa ya kusoma zaidi,hivyo aliwashauri kuwa na bidii ya kusoma kwa kadri ya fani wanayoimudu.

"Kwani katika wakati tulionao akina mama wakikosa elimu ya kutosha watakuwa na wakati mgumu katika kuzikabili changamoto zinazowakabili"mwisho wa kumnukuu.

Ukht Thuwaiba (ambaye pia ni mwanasheria wa Munira Madrasa) alikuwa ni mmoja kati ya wakhitimu waliotunukiwa Shahada ya Uzamili Uongozi na Utawala,mahafali ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Agha Khan Upanga Dar es salaam.

0 comments:

Post a Comment