Dec 12, 2013

KIJANA AJINYONGA

MFANYABIASHARA Musa Boazi (19), mkazi wa Kisukuru-Ukonga, amekufa kwa kujinyonga na kamba ya manila.
Boazi alikutwa amekufa juzi, saa 8 mchana maeneo ya nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema kuwa maiti ya mtu huyo ilikutwa ikining’inia nyuma ya mlango wa choo cha nyumba aliyokuwa akiiishi.

Alisema sababu za kujinyonga hazijafahamika, kwa kuwa marehemu hakuacha ujumbe wowote. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wakati huohuo, juzi zimekutwa maiti za watoto wawili wa kike na kiume wenye umri wa siku moja zikiwa ndani ya boksi zimetupwa na watu wasiofahamika maeneo ya Kigogo Dampo.

0 comments:

Post a Comment