Dec 12, 2013

Viongozi wa kidini watoa wito wa utulivu CAR

Viongozi wa kidini watoa wito wa utulivu CAR

iongozi wa kidini wametoa wito wa kuweko amani na maelewano kati ya Waislamu na Wakristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati huku vikosi vya jeshi la Ufaransa vikiendelea kupambana na waasi nchini humo.

Viongozi wa dini hizo mbili wamekutana mjini Bangui na kugawa chakula kwa zaidi ya watu 10, 000 waliokimbia mapigano huku wakiwasihi wasameheane. 

Imam Oumar Kobine Layana Mwenyekiti wa Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amewahubiria wafuasi wa Kikiristo na kusema kuwa, wao wote ni ndugu na hilo ndilo jambo muhimu zaidi. 
Ufaransa imetangaza kuwa, kuna wasiwasi wa kutokea mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kama yale yaliyotokea nchini Rwanda dhidi ya Watutsi mwaka 1994.

Mapigano yalizuka nchini humo baada ya wanamgambo wa Kikiristo kuanza kukabiliana na waasi wa zamani wa Seleka ambao ni Wasilamu ikiwa ni baada ya kupinduliwa Rais Francois Bozize kwa msaada wa waasi hao.

0 comments:

Post a Comment