Nov 23, 2013

TUUNGANE KUOKOA MAISHA YA BIBI HUYU


Ama kweli hujafa hujaumbika,ndivyo wanavyosema Waswahili.

Haya yana thibitishwa na hali halisi aliyo nayo Bi Mwajabu Muhamed mkazi wa Jangwani Maeneo ya Msimbazi Bondeni Jijini Dar es salaam.

Bi Mwajabu anayekabiliwa na ugonjwa wa kansa ulio sababisha kuoza kinywa chake na kupoteza muonekano halisi wa sura yake.
Mwandishi wetu alifanya mahojiano na bibi huyo mchana huu baada ya kukutana neye katikati ya jiji akitafuta Rizki,ambapo amesema maradhi hayo  yamemuanza miaka mingi.

Akiongea kwa taabu kubwa kiasi cha kushindwa kusikika vizuri alisema amefuatilia matibabu kwa kipindi kirefu bila mafanikio.

Akiwa kaambatana na Binti yake wa mwisho aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Hassan (36),amesema mama yake amepatwa na maradhi haya kabla hajamzaa.

"Nimeambiwa kwamba mama kanizaa akiwa na maradhi haya ambayo anayo hadi hivi sasa".

Akielezea mkasa huo Bi Rahma ambaye ni mtoto wa mwisho wa Bi maryam amesema"kwa mujibu wa historia aliyo nayo,mama yangu enzi za Usichana wake alipatwa na kichunusi kidogo pembezoni mwa mdomo",

Aliendelea kuhadithia kwamba mama yake alikipasua na kutoka uchafu mweupe ambao ni wa kawaida.

"Cha ajabu kikaanza kidonda na hatimaye kikawa kina kuwa siku hadi siku hadi kufikia hali hii unayoiona",alisema kwa masikitiko.

"Tumejitahidi kumpatia matibabu sehemu mbalimbali tukianzia Muhimbili,tukapelekwa Ocean Road ambapo alichomwa mionzi ishirini na hatimaye tukaenda Moshi katika Hospitali ya KCMC, hatujaona mafanikio yeyote"alisema.

Bi Rehema aliongeza kwamba "mama yangu anasumbuliwa na maumivu makali sana,huwa analia kama mtoto mdogo,hatuna cha kumpa zaidi ya kumpatia Panadol au Diclopa,lakani kwa sasa tuna tumia dawa za kisunna kwa ajili ya kusafisha kidonda,Mwisho wa kumnukuu.

Mwandishi wa habari hizi alikuwa na shauku ya kujuwa namna gani Mgonjwa huyo anaweza kula,ambapo alijibu kwamba chakula chake ni vitu laini laini na huwa anavitupia tu,kwani hawezi kutafuna.

Bi Rehema amewaomba wapenda kheri na wasamaria wema wamsaidie mama yake kwa kumtafutia matibabu nje ya nchi lakini pia wamsaide chakula. 

"Kwa kweli sipo tayari kuolewa,kwani nikiolewa nitakosa uhuru kamili wa kumuuguza mama yangu ambaye kimsingi anahitaji huduma za karibu sana kutoka kwetu watoto wake",alisema kwa huzuni Bi Rehema alipojibu swali la mwandishi wetu aliyetaka kujuwa kama ameolewa au yupo tayari kuolewa.

Munira blog ina waomba wapenda kheri na wasamaria wema kujitokeza kumsaidia Bi Mwajabu kwa hali na mali,kwani kwa kweli yupo katika mazingira magumu sana ya kupigania Uhai wake.ALLAH AMUA'FU IN SHAA ALLAH

KWA WATAKAO KUWA TAYARI KUWASILIANA NAO WATUMIE NAMBA IFUATAYO 0714 36 36 46 (NAMBA HII NI YA REHEMA HASSAN AMBAYE NI MTOTO WA MWISHO WA BI Mwajabu).

 BI MARYAMU KUSHOTO AKIWA PAMOJA NA MWANAWE BI REHEMA HASSAN WAKATI WAKIFANYA MAHOJIANO NA MWANDISHI WA MUNIRA BLOG MCHANA HUU.

0 comments:

Post a Comment