Nov 12, 2013

Tutapambana na Magaidi-Pinda



somalimemo.net 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema Serikali kupitia polisi inaendelea kujipanga kukabiliana na matishio mbalimbali ya usalama, ukiwamo ugaidi.

Akitoa hoja ya kuahirisha Bunge Dodoma hivi karibuni, Pinda alisema matukio ya hivi karibuni nchini Kenya na kukamatwa kwa watuhumiwa nchini ni ishara kwamba ugaidi hauna mipaka unaweza kutokea nchi yoyote.

Pinda alirejea matukio ya kukamatwa kwa vijana wa 12 waliokuwa mkoani Mtwara na wale waliokamatwa Wilaya ya Kilindi wakiwemo wanawake na watoto,mkoani Tanga, kuwa ni ushahidi unaotoa wajibu wa kuimarishwa kwa ulinzi na kuchukua tahadhari dhidi ya matukio hayo.

“Kila kiongozi wa eneo ajue watu wanaoishi katika himaya yake. Kazi hii itasaidia kuepuka tatizo la wageni wasiojulikana au wahamiaji haramu,” alisema Pinda.
na kuongeza:
“Aidha kamati za Ulinzi na Usalama za mitaa na vijiji zinahimizwa kutekeleza mkakati wa kuzuia uhalifu kwa kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi, kwa kuzingatia sheria ya serikali za mitaa na sheria ndogo zilizotungwa ili kuimarisha usalama katika halmashauri husika”.
Alisema Serikali imekuwa ikiwahimiza wafanyabiashara wasaidiane na vikundi vya ulinzi shirikishi huku wale wenye biashara kubwa zenye mikusanyiko ya watu wengi wanaagizwa kufunga kamera za usalama na kuziunganisha kwenye mtandao wa polisi ambao wanaweza kutoa msaada pale uhalifu unapotokea.

0 comments:

Post a Comment