Nov 12, 2013

Sheikh Mohamed Issa "mimi sio kiongozi wa kuulizwa mauaji ya Kilindi!"

somalimemo.net 

Mauaji yaliofanyika katika vijiji vya waislaam huko Kilindi vimenyamaziwa kimya na Mashekhe wengi,na baadhi yao siku za nyuma walikuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya Habari na kutunisha misuli kwa masuala yasio na manufaa kwa waislaam badala ya kuzungumzia madhila na mauaji yaliofanywa na yanayoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini Tanzania.

lakini kadhia hii ya mauaji ya Kilindi na mahauji ya waislaam imenyamaziwa kimya na kufikia hatua kuwa baadhi ya Mashekhe ukigusia kuuliza kadhia hizo wamekuwa wakali kwa waislaam.
Ndugu yetu katika Iman hivi punde alifanya mahojiano Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Baraza la Wanazuoni Hey-At Ulamaa Tanzania Sheikh Mohamed Issa.

YALIYOMO JUU YA BAADHI YA MASHEIKH WA TANZANIA JUU YA KADHIA YA KILINDI.
Ndugu zangu waislam suala zima la mji wa kilindi limekuwa gumu kupata habari zake,na wala hatukuweza kuwasikia masheikh nchini tanzania wakilizungumzia jambo hilo huku damu za waislam zikiwa zimemwagika.

Mahojiano yalifanyika hivi:-
Mwulizaji:-assalam alaykum sheikh mohammed issa.
Sheikh Mohamed Issa:-waalaykum salaam.


Mwulizaji:-niliikuwa nataka kujua kuhusiana na suala la kilindi sijui mmechukua hatua gani nyie viongozi.
Sheikh Mohamed Issa:-mimi nimeingia leo nimetoka nje na mimi sio kiongozi, wewe umenichagua mimi ukajua mm ni kiongozi,unajua mimi ninachokula kama umenichagua mm kiongozi,kwanini wewe usifatilie wewe umechukua juhudi gani.?



Mwulizaji:-sisi tunataka tujue kuna kauli gani kutoka kwenu nyie viongozi
Sheikh Mohamed Issa:- mimi sio kiongozi unajua mm nachokula,kwanza simu zetu zinarekodiwa,mnakaa nyie na wake zenu
nyumbani hamjui familia zetu zinakula nini alafu mnataka sisi tuwe wasemaji?


Mwulizaji:-sheikh mohammad issa kumbuka mtume (Swal lahu aleyhi wasalam) amesema itafika siku waislam watagombaniwa na makafiri kama chakula maswahaba wakauliza kwa uchache wetu ya rasullallah mtume akasema mtakuwa wengi lkn wengi wenu mtakuwa km takataka za mapovu ya bahari maswahaba wakauliza kwann iwe hivyo mtume akasema mtasalitishiwa wahann maswahaba wakauliza nn wahhan ya rasulla llah mtime akajibu ni kupenda dunia na kuchukia mauti.



Sheikhe akauliza hii hadith ilikuwa makka au madinna akajibiwa madinna akasema sisi hali tulokuwa nayo sasa ni hali ya makka hatuna nguvu kwa hiyo hatuwezi kupambana na makafiri tunachofanya ni kuwaandaa waislam kwa ajili ya siku za mbele.hata km sisi tukiwa tumefa.na kutoa mfano wa kisa cha ammar bin yassir.


Kukawa na majibizano makali na kukubali yeye ni kiongozi na wanawawekea mawakili watu wa kilindi huku akijibu walouliwa allah ndio anajua kuhukumu.


Subhannallah hii ndio hali halisi tulonayo waislam tanzania.


Chanzo cha habari ni kutoka vyombo vya habari somalia.

0 comments:

Post a Comment