Nov 12, 2013

Serikali ya Kenya yafunga Madrasa za Kislaam.



somaliamemo.net 

Viongozi nchini Kenya wameanza kuyafunga vituo kadhaa vya elimu ya dini inayomilikiwa na waislaam wanaoishi katika nchi humo iliyoko Afrika mashariki.

Tangu kutokea shambulio la Westagte mwezi October mwaka huu mashrika ya Usalama ya kupambana Ugaidi nchini Kenya wameanza kuwawekea vikwazo kadhaa kwenye Madaris na misikiti za waislaam wa nchi hiyo wakidai kuwa zinafundisha msimamo mkali na Ugadi.

Habari kutoka wilaya ya Galgal iliyopo Counti ya Nakuru zinaeleza kuwa Maofisa kadhaa wa kupambana na ugaidi waliingi kwa nguvu Madrasa ya Kislaam iliyopo wilayani hapo ambapo waislaam wa kenya walikuwa wakipata mafunzo ya Dini.

Afisa moja wa Usalama aliyekataa kutaja jina lake ameliambia gazeti la Standard la nchini Kenya kuwa wameyafunga madrasa kadhaa za Dini za Kislaam na kuongeza kuwa Madrasa hizo zilikuwa zikifundisha vijana kwa kile alichokiita "Manhaj ya Kiwahabi" akiwa na maana aqida swahihi ya Kisalafi.

Kiongozi mkuu wa Elimu wa County ya Nakuru Mathew Ambuka amesema "Serikali ya Kenya inapambana vikali na Manhaji ya Kiwahabi na kwa hivyo tumeyafunga Baadhi ya Vituo vya Kidini ambazo hazikusajiliwa na Wizara ya Elimu ya Kenya,Serikali ya Kenya inakubali ufunguaji na kujenga Mashule za Kislaam ambazo ni za mrengo wa kati na pia za Kisufi."

Serikali ya Kenya inadai vijana wa Kislaam waliokuwa wakijifunza Mafunzo ya Dini ya Kislaam mwaka jana walivuka na kuingia kujiunga na Al-Shabab wanaopigana nchini Somalia.

0 comments:

Post a Comment