Oct 11, 2013

SHEIKH AZZAN aanza Matibabu,aendelea Vizuri.



Hatimaye sheikh Azzan ameanza kupata matibabu nchini India.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka nchini India vinasema,sheikh Azzan ameanza matibabu hayo baada ya kupatiwa vipimo.

"Ameanza matibabu,imeonekana katika mafigo yake kuna vijiwe kumi na saba na jana vimeyeyushwa vijiwe vya upande wa kushoto na baada ya wiki moja vitayeyushwa vijiwe vya upande wa kulia",kilisema chanzo chetu.

kiliendelea kusema "kwa sasa Al hamdu lillah hali inaridhisha tofauti na hapo awali kwani alikuwa na maumivu makali sana kiasi cha kupoteza fahamu".

Kikieleza zaidi chanzo chetu kilitupasha kwamba kwa sasa kabakisha vipimo viwili kwa maana kipimo cha kichwa na kipimo cha tumbo.

"Tunataraji atarudi katika hali ya kawaida kwa uwezo wa ALLAH muhimu afuate masharti aliyopewa na  Daktari"Kilikhitimisha kutujuza chanzo chetu.

Sheikh azzan ni mmoja miongoni mwa viongozi ya Jumuiya ya Uhamsho Visiwani Zanzibar,alisafirishwa wiki iliyopita kwenda nchi India kwa ajili ya kutibiwa,baada ya kuzidiwa akiwa gerezani.

Mwishowe Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilimpa kibali cha kwenda kutibiwa baada ya kupata dhamana ya mahakama.

Munira blog inamtakia Afya njema.

0 comments:

Post a Comment