- ASKARI WENZAKE WAMLAUMU.
- WAISLAMU MOROGORO WAIKATAA TUME,WASHANGAZWA MUHALIFU KUINGIZWA KATIKA TUME.
- WAELEZEA FILAMU MZIMA YA TUKIO LILIVYOTOKEA.
Na mwandishi wetu wa munira.
Waislamu mkoani Morogoro wamesema wanamjuwa Askari Polisi aliyempiga risasi Sheikh Ponda Issa Ponda mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akiongea kwa njia ya simu mapema leo hii Sheikh Abeid Haroub amesema "kwa kweli inauma sana kuona kwamba tunafanywa kama watoto wadogo,tunanyanyaswa,tunafanyia ukatili,tunafanyiwa unyama hali ya kuwa sote ni watanzania".
Aliendelea kusema "kwanza naomba ufahamu nazungumza nikiwa ni mtetezi wa haki za Binaadamu,siwezi kuufunga mdomo wangu ninapoona au kufahamu kuna binaadamu anafanyiwa au kafanyiwa ukatiri ambao ni kinyume na haki za binaadamu,Sheikh ponda kapigwa risasi na Askari Polisi aliyempiga risasi anayeitwa Benadect,kapigwa eneo la gereji katika kona ya barabara ya Tumbaku,hii ni baada ya gari moja la polisi (miongoni mwa magari mengi) kulizidi kasi gari alililopanda Sheikh Ponda.
Akisismulia mkasa huo Sheikh Abeid alisema "waliomba kibali jeshi la polisi kwa ajili ya kufanya mhadhara nao wakaridhia kuwepo kwa mhadhara huo wenye sura la Baraza la Idd,tukiwa tupo katikati ya mhadhara tukaona magari ya polisi yamekuja,tukajuwa wamekuja kama ilivyo kawaida ya kuimarisha ulinzi penye mkusanyiko wa watu wengi,lakini kadri muda ulivyozidi kusonga idadi ya magari ya polisi na askari polisi iliongezeka,mara wakaanza kupeperusha bendera nyekundu,hii ikawajengea hofu akina mama na watoto wakaanza kutaharuki,mhadhara ulipokwisha ndipo waislamu na Sheikh Ponda kuanza kuondoka nao Askarai wakaanza kumfuata,hali hii ikapelekea waislamu nao kushawishika kumsikndikiza Sheikh Ponda,ilipofika kona ya barabara ya tumbaku eneo la gereji gari moja ya polisi ikalipita gari la Sheikh Ponda na kulizuwia kwa mbele,hali hii ilimfanya Sheikh Ponda kushuka na kusogea pembeni mara Askari Polisi anayetwa Benadict aliyeshika Bastola akafyatua risasi na kumpiga Sheikh Ponda na kuanguka chini,Sheikh Ponda akajaribu kuinuka,akashindwa akajaribu tena akashindwa ndipo wasamaria wema wakamnyanyua,alisikika askar polisi mmoja akisema sasa umeshaharibu kwa nini umemshut,"Mwisho wa kumnukuu.
Kwa upande wake kijana mmoja aliyekataa kutaja jina lake ambaye anafanya kazi katika Gereji hiyo alisema "mara baada ya kumpiga risasi afande benadect alikuja na kutuuliza,hamujamuona mtu aliyevaa kanzu kapita hapa,sisi tulimkatalia (japo tulimuona sheikh ponda akiwa amebebwa bila ya sisi kujuwa kwamba yeye ndiye ponda),siku ya pili alikuja Benadict na wenzake kutafuta ganda la risasi,lakini cha kushangaza siku chache baada ya tukio hilo walikuja watu wakidai kwamba wao ni tume ya kuchunguza tukio hilo na kutaka kutuhoji juu ya tukio hilo,lakini katika watu hao yule askari polisi Benadect naye yupo huku akitukazia macho,katika mazingira hayo utafanya nini,yaani bro sijuwi hii inchi tunaipeleka wapi"mwisho wa kumnukuu kijana huyo.
Katika hatua nyengine waislamu wa mkoa wa morogoro wamekataa kuhojiwa na tume hiyo kwa madai ni tume ya kulitakasa jeshi la polisi na si tume huru ya kuchunguza
tukio lakupigwa risasi sheikh ponda,
"Leo mualifu unamuingiza katika tume,unatarajia nini kama si kiini macho"alisema sheikh abeid.
Muda mfupi uliopita mwandishi wa blog ya munira alimpigia simu kamanda wa polisi mkoa wa morogoro shilogile ili kuthibitisha juu ya madai ya askari polisi Benadect kuingizwa katika tume au kwenda nae eneo la gereji ya barabara ya kona ya tumbaku ili kuwahoji walioshuhudia,kamanda shilogile alisema "mimi sipo katika tume na hata waliopo katika tume siwajuwi kwa hiyo siwezi kuizungumzia tume,chukua namba hii umpigie mwenyekiti wa tume atakuwa na majibu ya maswali yako"
munirablog ilipojaribu kumpigia,hali ilikuwa hivi,"samahani,namba ya mteja unayompigia,haipo."