Aug 10, 2013

TUUNGANISHE NGUVU KUWAKOMBOA MASHEIKH WALIOPO MAGEREZANI-SHEIKH PONDA.


  • ASEMA NI UNYAMA MKUBWA MNO ULIOPO ZANZIBAR 
  • WANADHALILISHWA NA KUNYANYASWA.
  • WANAONANA NA FAMILIA ZAO KWA TAABU.
  • AVITUPIA LAWAMA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KWA UPOTOSHAJI.


Na waandishi wa munirablog;
Waislamu wa Tanzania wametakiwa kuunganisha nguvu ya pamoja kuwakomboa Masheikh na Waislamu wengine takriban wapatao khamsini walioko magerezani visiwani Zanzibar na hapa Tanzania bara.

Wito huo umetolewa jana na katibu wa kamati ya kutetea Haki za waislamu Tanzania sheikh ponda issa ponda alipokuwa anawahutubia waislamu waliofurika katika msikiti wa kichangani ikiwa ni katika sherehe za baraza la idd.

"Amesema nimekwenda Zanzibar,nimekaa kwa siku tatu nikapita katika magereza ambayo Masheikh wetu wamezuiwa,nikakutana nao,nikaongea nao,kwa hakika kwa mujibu wa maelezo yao na kwa namna nilivyowaona,ni dhahiri ya kwamba wanafanyiwa unyama wa hali ya juu, wanadhalilishwa,wananyimwa haki za msingi,sasa hawa ni ndugu zetu tena sote tupo katika taifa moja,ni lazima tuunge nguvu zetu kuhakikisha tunawakomboa,kwani kilichopo hivi sasa ni dhulma ya wazi ambayo hatupaswi kuivumilia".mwisho wa kumnukuu.

Hakuna sababu ya msingi inayopelekea masheikh wetu hadi leo hii wawe magerezani,kwani wameuwa?hata hao waliokamatwa kwa tuhuma za mauwaji sasa wako njee,ndugu zangu hakuna njia ya itakayo tusaidia ila ni kuunganisha nguvu zetu sisi waislamu wa bara na waislamu wa Zanzibar kuhakikisha tunawakomboa ndugu zetu hawa.

“Hili tatizo haliishii kwa masheikh na maimau wetu tu,bali hata maamuma nao wankoseshwa haki za msingi za kuwasikiliza masheikh wao ambao wapo magrezani,ndugu zangu hebu fikirini,sheikh farid,sheikh mselem na wengineo,hawa wana darsa zao wanawafundisha waumini wao lakini katika mwezi mzima wa ramadhan darsa hizi hazikuendeshwa kwa kuwa masheikh wao wapo ndani,sasa hii ni dhulma isiyovumilika”alisema

Kwa upande mwengine Sheikh ponda alivilaumu baadhi ya vyombo vya habari kwa kupotosha ukweli,"mimi nilikwenda Zanzibar na nimekaa kwa siku tatu,nilikuwa natembea barabarani tena kwa miguu,nimeswali katika misikiti mbalimbali,nimekwenda kuwaona masheikh wetu waliopo magerezani,halafu baadhi ya vyombo vya habari eti vinasema nimejificha na vyengine vinasema nimekimbia,huu ni upotoshaji." aling'aka Sheikh Ponda.

Tunawaomba ndugu zetu wa habari,waripoti matukio kwa uhalisia na si vinginevyo.

Kumekuwa na wimbi la kuwakamata na kuwasweka ndani masheikh na waislamu kwa madai mbalimbali na hata kuwanyima dhamana au kuweka masharti magumu ya dhamana kitu ambacho waislamu wanahisi ni uonevu dhidi yao.

 HAWA NI BAADHI YA WAUMINI WALIOFURIKA KATIKA MSIKITI WA KICHANGANI JANA KUFUATILIA BARAZA LA IDD