Jul 14, 2013

LENGO NI KUWAFANYA WATOTO WAITHAMINI NA KUIFANYIA KAZI QUR AAN-TIPSO


  • YAFANYA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR AAN,
  • MSHINDI KUPATA PESA TASLIM NA KULIPIWA ADA YA SHULE.

Na mwandishi wetu wa munira.
Jumuiya ya wanafunzi wa shule za msingi za Kiislamu Tanzania (TIPSO) kwa kushirikiana na kamati ya mashindano ya kuhifadhi Qur aan leo hii inafanya mashindano ya kuhifadhi Qur aan kwa wanafunzi wa shule za msingi za Kiislamu Tanzania.

Mashindano hayo yanaendelea kufanyika leo hii katika ukumbi wa Diomond Jubile uliopo upanga Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na mwndishi wa munirablog,katibu wa kamati ya mashindano hayo Sheikh  Mzee Mwinyikai alisema "tumeamua kuandaa mashindano haya kwa lengo la kuwahamasisha wanafunzi  wanaosoma katika shule za msingi za Kiislamu kuithamini,kuipenda na kuitumika Qur aan,tunahitaji watoto hawa waishi kwa mujibu wa Qur aan sasa ili tufanikiwe hilo ni lazima tuwahamasishe kuijuwa,kuihifadhi na kisha kuipenda",alisema mwinyikai.


Aliongeza kwa kusema kwamba mbali ya lengo hilo kuu,lakini pia mashindano hayo yana lengo la kuleta upendo,umoja na kufahamiana zaidi.

Aidha alisema kuwa washindi wa katika kila kundi watalipiwa Ada ya mwaka mmoja na watapewa pesa taslimu ambazo zitatolewa na kamati ya zakakah na swadaqah ya D Y C C C.

katika mashindano hayo mgeni Rasmi alitarajiwa kuwa ni Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe Azzan Zungu ambaye kwa mujibu wa habari zilizotufikia hivi punde tayari kesha fika katika ukumbi huo.

Hadi mwandishi wa munirablog anaondoka katika eneo la tukio mashindano hayo yalikuwa yameshaanza na yanaendelea.

munirablog inawahidi wasomaji wake kuwapatia matokeo ya mashindano haya mara tu yatakapo malizika Inshaa Allah 

HABARI NA MATUKIO KATIKA PICHA


Mwanafunzi Jamil Muhammad Hariz wa shule ya Yemen akisoma Qu raan katika mashindano ya kuhifadhi qur aan yaliyoandaliwa na TIPSO kwa kushirikiana na kamati ya mashindano ya kuhifadhi Qur aan Tanzania.
mashindano haya yanafanyika hivi sasa (yanaendelea) katika ukumbi wa Diomond Jubilee

MWANAFUNZI  HUSSEIN SAID WA SHULE YA AL HIKMA AKITIMIZA WAJIBU WAKE KATIKA MASHINDANO HAYO YANAYOENDELEA KATIKA UKUMBI WA DIOMOND JUBILEE.

 HAWA NI BAADHI YA WAUMINI WALIOJITOKEZA KUSHUHUDIA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR AAN YANAYOENDELEA KATIKA UKUMBI WA DIOMOND JUBILEE. 

 PICHA ZA WASHINDI ;




 Hawa ni washindi wakiwa na mgeni rasmi pamoja na viongozi wa TIPSO