Jun 30, 2013



KATIKA KUUKARIBISHA MWEZI WA RAMADHANI,WAISLAMU WASHAURIWA

TUKIMBILIE FURSA ZINAZOPATIKANA KATIKA MWEZI WA RAMADHAN.

  • TUMFANYE SHAITWANI KUWA NI ADUI YETU.
  •  TUSIPOTEZE MUDA KWA MAMBO YASIYOFAA.

Na mwandishi wetu wa munirablog.

Waislamu wametakiwa kuzichangamkia na kuzitumia kikamilifu fursa zinazopatikana katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao unatarajiwa kuanza wiki ijayo Inshaa Allah.

Hayo yamesemwa na Sheikh Ramadhan Khamis Kwangaya kutoka Taasisi ya HAY-ATUL ULAMAA yenye makao yake Jijini Dar es salaam.

Ameyasema hayo usiku huu wakati akitoa mada ya Fursa na Changamoto zilizopo ndani ya Mwezi wa Ramadhan ikiwa ni muendelezo wa mihadhara ya kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan inayoandaliwa na kamati ya mihadhara ya Masjid Qiblatain.

Akiwahutubia Waislamu wa Masjid Tawwab wa Magomeni Makuti Manispaa ya Kinondoni Jijini
Dar es salaam,Sheikh Kwangaya alisema uwepo wa mwezi wa Ramadhan ni Fursa pekee kwa muislamu kuitumia vizuri Ofa nono aliyoiweka MwenyeeziMungu kwetu.

“Kwa siku tunafunga masaa yasiyozidi 14,utakapoifunga vizuri fahamu utalipwa thawabu kwa kila sekunde moja,na thawabu katika mwezi wa Ramadhan zinazidishwa hadi kufikia mara sabini (70) sasa malipo haya unayapata hapa duniani huku faida ya malipo haya utayakuta Akhera kwa wewe kuwekwa mbali na moto wa Jahannamu kwa zaidi ya miaka 1,500,000”.

Aliwatanabaisha waislamu kwamba Thawabu hizi atazipata yule aliyefunga kikamilifu kwa maana kufunga tumbo lake na viungo vyake huku akisema kufunga kinyume cha hivyo ni khasara kwa mfungaji huku akinukuu maneno ya Mtume s,a,w aliposema yawezekana mfungaji asiambulie chochote zaidi ya kushinda njaa na kiu.

Alisema tukizitumia vizuri fursa hizi ndani ya mwezi wa Ramadhan hatutokuwa na sababu za kukosa Radhi za Mwenyeezi Mungu.

Aidha aliwaasa waislamu kuzikabili changamoto zinazopatikana ndani ya mwezi wa Ramadhan kwa kuanza sasa kumfanya Sheitwani kuwa ni adui yetu.

Ndugu zangu waislamu tufahamu ya kwamba Mtume s,a,w aliposema ya kwamba Funga ni kinga,Shaitwani alilifahamu neon hili vizuri sana,ndipo akaweka mipango mikakati dhidi ya waislamu,mipango hii ameigawa sehemu mbili,sehemu ya kwanza ni kumshawishi na kumlaghai muislamu afanye maasi sana kabla ya kufunga na sehemu ya pili ni kumshawishi na kumlaghai muislamu afanye maasi siku za mwanzo tu baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani”,mwisho wa kumnukuu.

Aliendelea kusema,”hakuna mwezi ambao baadhi ya waislamu wanafanya maasi sana kama katika mwezi huu wa shaaban hasa katika siku za mwisho wa shaaban,na mwanzoni mwa mwa mfungo mosi,ndiyo maana kila kona utasikia kwamba kuna vunja jungu wakimaanisha kufanya maasi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza kwa mfungo wa Ramadhan,shaitwani kawapambia haya kwa kuwa anajuwa fika kwamba ukianza Mwezi wa Ramadhan yeye anafungwa minyororo.”alisema.

Huku waumini wa kiislamu wakiendelea kumsikiliza,Shekh Kwangaya alisema,ukiingia katika ibada ya swaumu hali ya kuwa tayari umeshajipakatisha madhambi una athirika kifikra na kiimani na uwezo wa kufanya ibada kwa umakini unakosekana,sasa hapa shaitwani atakuwa kafanikiwa lengo lake.

Aidha aliwafahamisha waislamu ya kwamba mpango mkakati wa pili wa shaitwani dhidi ya waislamu ni kumfanya muislamu amuasi Mungu mara tu baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani ili aiharibu funga yake yote ya mwezi mzima.

Aliwakumbusha waislamu kwamba lengo la kufunga ni kumfanya mtu afikie daraja la Ucha Mungu na maana ya Ucha Mungu ni mtu kujitenga na kujiepusha na maasi yote.

Aliwashauri waislamu kufanya wingi wa Swala za usiku,Swala za kablia na baadia,kusoma Qur aan,kuleta adhkaar,kuwahi msikitini kwa lengo la kuisubiri Swala,na kukaa msikitini baada ya swala,matendo haya yanafaida kubwa sana kwetu hasa ndani msimu wa mwezi wa Ramadhan.

Kamati ya maandalizi ya mihadhara ya Masjid Qiblatain chini ya uenyekiti wa Sheikh Ally Bassaleh imekuwa na desturi ya kuandaa mihadhara ya aina hii kwa kila mwaka na kuwapa faida nyingi waislamu,ambapo kesho mhadhara utakuwa katika Msikti wa Mtoro na mhadhiri atakuwa Sheikh Nurdin Kishki,Inshaa Allah blog ya munira itakuwepo na itawahabarisha.


0 comments:

Post a Comment