Jun 30, 2013

Sheikh.Kilemile- Tuzihuishe Darsa za Mtume [S.A.W]



  • Zimezalisha masheikh wengi.
  • Qur aan ingekuwa ijifafanuwe yenyew isingebebeka.



Na mwandishi wetu wa munirablog.

Waislamu nchini kupitia misikiti mbalimbali wametakiwa kuzihuisha darsa za Mtume s.a.w. kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanatekeleza sunna ya mtume s.a.w.



Wito huo umetolewa jana baada ya Swala ya Maghrib na Sheikh Suleyman Amran Kilemile alipokuwa ana zungumza na Waislam katika hafla fupi ya kusheherekea kutimiza miaka kumi na tatu ya uwepo wa darsa ililoambatana na shindano la Hadithi katika msikiti wa Kipata uliopo Kariakoo Jijini Dare s salaam.



Alisema "Qur aan ingekuwa ijifafanuwe yenyewe pasipo kuwepo kwa Hadithi (maneno ya Mtume s.a.w.) ni dhahiri isingechukulika.lakini Mwenyeezi Mungu kwa Hekima zake akamfanya Mtume s.a.w. kuwa ni mtafsiri wa Qur aan hiyo kupitia maneno yake'.



Alizinukuu Aya mbili (43 na 44) zilizopo katika Surat Nnahli kuwa ni Aya zinazo thibitisha hilo na kusema “wanaodai waishi na qur aan pekee hawa wanazipinga Aya hizi”



Kwa kipindi kirefu tulielekeza nguvu zetu kutafsiri Qur aan pekee tukasahahu kwamba hadithi ndiyo sunna yenyewe lakini kwa masheikh wachache kama hawa kuendesha Darsa za Hadithi kwa kweli wamefanya jambo la maana sana” alisema.



Alionesha masikitiko yake kwa baadhi ya misikiti kutokuwa na Darsa mbalimbali zikiwemo za Hadithi na kumfanya atoe wito kwa maimamu na masheikh mbalimbali kuzianzisha na kuzisimamia Darsa katika misikiti yao.



Hizi darsa zinazo endeshwa baina ya maghrib na ishaa kwa kweli zimezalisha masheikh wengi hapa bara na kule Zanzibar,tunapaswa kuziendeleza kwa zile zilizopo na kuanzisha nyengine kwa misikiti ambayo haina darsa hizo tena ikibidi hata waumini na viongozi wa misikiti wamwatafute masheikh wanye uwezo wa kusomesha Darsa hizo”,mwasho wa kumnukuu.



Awali akitoa maelezo yake Mwalimu wa Darsa hiyo Sheikh Abdallah Ahmad Bawazir alisema Darsa hiyo ameianzisha mwaka 2000 baada ya kuombwa na viongozi wa msikiti huo ambao wengi wao wameshafariki.



“Tayari nimeshafundisha kitabu chote cha umdatul ahkaam,buluughul maraam,na sasa tunaendelea na kitabu cha sunan abii daaud”Alisema sheikh Bawazir.



Alieleza lengo la shindano hilo ni kukuza na kuimarisha maarifa ya vijana ambapo vijana 18 (kati ya vijana 37 waliochukuwa fomu ) kutoka mikoa mbalimbali walishiriki Shindano hilo huku mshindi atakayepata kwa asilimia mia moja akiahidiwa zawadi ya pesa taslim Shilingi laki tano (500,000).



Kwa bahati mbaya hakupatikana mshindi kwa kujibu sawa sawa kwa asilimia mia moja.



Pamoja na hivyo wadhamini wa Darsa hilo waliwazawadia washindi pesa taslim kwa viwango tofauti kwa lengo la kuwahamasisha.



Washindi hao ni Abdallah Said Madijimba (Iringa),Abuu Hanifa Said Bakar (Tanga),Abuu Muhammad Ahmad (Iringa),Hafswa Nassoro Ahmad (Dare s salaam) na Omar Kulili (Dar es salaam).



Sheikh Abdalaah Bawaziri ni mahiri katika fani ya Hadithi na kwa sasa ana miaka 35 tangua aanze kazi ya kufundisha Somo la Hadithi katika misikiti mbalimbali hapa nchini.



Kwa sasa anaendesha Darsa za Hadithi katika misikiti ya Kipata na Qiblatain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es salaam.

 Sheikh Kilemile akimkabidhi Sheikh Bawazir Zawadi maalum iliyoandaliwa na wanafunzi wa Darsa hilo linaloendeshwa katika msikiti wa kipata,hafla hiyo ya kutimiza miaka 13 ya uwepo wa Darsa hilo ilifanyika jana baada ya swala ya magrib.

 Sheikh Suleyman Amran Kilemile akimkabidhi zawadi mmoja ya washindi wa Shindano la Hadithi lililofanyika jana katika Msikiti wa Kipata jijini Dar es salaam.


0 comments:

Post a Comment