Kaimu
Kamishna wa TRA Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo
pichani) katika mkutano wa kuota taarifa juu ya ukusanyaji wa kodi kwa
mwezi Februari.
Serikali
ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya
Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na
malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa akifafanua kuhusu juhudi za
Serikali katika kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu
kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.
“ Napenda
kuwaambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali
watu wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda Mamlaka moja ya
utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya
mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya
wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema
Kidata.
“Kamishna
Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo
imechaguliwa na wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika
jambo lolote lile hivyo basi kwa sasaserikali ipo katika mchakato wa
kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo
wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi
wanazozifanya.
Kamishna
huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine
zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia
ufumbuzi suala la kero ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata
muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote
iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi
ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo
zimekuwa kero na hazina tija.
Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu
Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo hayatokani
na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri
zote nchini.
0 comments:
Post a Comment