MAMLAKA ya Usafiri Baharini Zanzibar imefuta safari zote za baharini siku ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, Machi 20 mwaka huu kutoa fursa kwa wananchi wenye sifa kupiga kura visiwani humo.
Katika taarifa yake jana, mamlaka hiyo ilisema siku hiyo ni marufuku kwa vyombo hivyo kusafirisha abiria kwa vile hiyo ni fursa pekee kwa wananchi kushiriki uchaguzi huo.
Taarifa hiyo ilisema uamuzi huo umefikiwa kutokana na wananchi wengi kujiandikisha kupiga kura.
Machi 20 mwaka huu wananchi wa Zanzibar watachagua viongozi wa ngazi mbalimbali baada ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana kufutwa kwa kile kinachodaiwa kuwa kasoro wakati wa upigaji kura.
Matokeo hayo yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Baadhi ya vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi huo wa marudio kikiwamo chama kikuu cha upinzani cha CUF.
0 comments:
Post a Comment