TANZANIA ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho kwa viwango vya furaha duniani.
Hiyo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Viwango vya Furaha duniani ya 2016 ambayo ilitolewa Rome, Italia jana wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa ya Furaha Duniani Machi 20.
Nchi nyingine ambazo zimo kwenye kundi hilo ni Madagascar, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria ,huku Burundi ikishika mkia.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana, ilisema orodha hiyo iliandaliwa kwa kuzingatia pato la mtu kila mwaka.
Mambo mengine yaliyozingatiwa ni miaka ambayo mtu anatarajia kuishi, mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwapo uhuru wa kufanya uamuzi, uhuru kutoka kwa ufisadi na ukarimu katika jamii.
Takwimu zinaonyesha Tanzania imeshika namba 149 kati ya nchi 157, ikiwa na alama 3.695 kati ya alama 10 na Rwanda ni ya 152 ikiwa na alama 3.315.
Uganda ni namba 146 na alama 3.739, Malawi ya 132 na alama 4.156, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeangukia namba 125, ikiwa na alama 4.272, wakati Kenya imeshika namba 122 ikiwa na alama 4.356 na Somalia ndiyo kinara kwa kuwa namba 76 ikiwa na alama 5.44.
Orodha hiyo imetayarishwa na Shirika la Maendeleo Endelevu la Sustainable Development Solutions Network (SDSN) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa.
Nchi 10 bora zinaongoza kwa furaha duniani ni Denmark ikiwa na alama 7.526 ikifuatwa na Uswisi, Iceland na Norway.
Nyingine ni Finland, Canada, Uholanzi, New Zealand, Australia na Sweden zinafunga 10 bora.
Ripoti hiyo imeonyesha Marekani inashika nafasi ya 13 duniani wakati Uingereza ipo nafasi ya 23.

0 comments:
Post a Comment