Mar 17, 2016

Sheikh wa al Azhar: Shia na Suni na mbawa mbili za Uislamu

Sheikh wa al Azhar: Shia na Suni na mbawa mbili za Uislamu
Sheikh Mkuu wa al Azhar nchini Misri amesema kuwa Shia na Suni ni wafuasi wa dini moja na ni mithili ya mbawa mbili za ndege mmoja 
 
Sheikh Ahmad al Tayyib amesisitiza kuwa, uhusiano wa Waislamu wa Shia na Suni ni mzuri na kwamba wafuasi wa madhehebu hizo mbili hawawezi kukufurishana na kuondoana katika dini. 

Sheikh Mkuu wa al Azhar ametahadharisha kuhusu harakati zinazolenga kuzusha mifarakano kati ya Waislamu na kusema kuwa, mifarakano ya kimadhehebu ni miongoni mwa hatari kubwa zinazozisumbua baadhi ya nchi za Waislamu za Kiarabu. 

Vilevile al Tayyib ameongeza kuwa, njama zinazofanyika kwa shabaha ya kuuhusisha ugaidi na dini ya Uislamu ni dhulma ya wazi dhidi ya dini hiyo ya Mwenyezi Mungu na ameyataka makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka inayochafua jina la dini na historia ya Umma wa Kiislamu kuondoka katika njia hiyo na kurejea katika njia sahihi. 

0 comments:

Post a Comment