Raia kumi wa Kenya wameituhumu Serikali ya Tanzania, kwa kukamatwa kwa kuwateka jijini Maputo nchini Msumbiji Januari 2006, ambako walikuwa wakiishi kihalali wakitafuta fursa za biashara, na kisha kuwapakiza kwenye ndege ya kijeshi na kuwaleta nchini Tanzania kwa nguvu.
Tanzania inasema watuhumiwa hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuletwa kupitia ndege ya jeshi la Msumbiji.
Wakenya hao wanahoji kuwa kesi yao nchini Tanzania imechukua muda mrefu kwa kuahirishwa mara kwa mara bila sababu.
Aidha wanadai kuwa kesi imeendeshwa bila wao kuwa na mawakili wa kuwatetea.
Mawakili wa serikali ya Tanzania pia waliieleza Mahakama ya Afrika kuwa, wawili kati ya raia hao wa Kenya waliofariki wakiwa magereza, walikufa kwa kifo cha kawaida, na kesi iliahirishwa mara kwa mara kutokana na mawakili wa walalamishi kukosa kufika mahakamani siku za kesi.
Wakenya hao walikamatwa miaka kumi iliyopita na kuhukumia kufungwa miaka thelathini jela, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji na ujambazi wa kutumia silaha lililofanyika katika benki ya NMB Tawi la Moshi, mwezi May,2004.
Mahakama ya Africa kuhusu haki za binadamu na za watu iliundwa mwaka 2006 na kuanza kazi zake rasmi mwaka mmoja baadae.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi februari 2016, Mahakama imepokea kesi 74, ambapo 25 kati ya hizo zimekwisha shughulikiwa, huku kesi 4 zikipelekwa katika Tume ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu nchini Gambia.
0 comments:
Post a Comment