Mahakama Maalumu ya Jinai ya Rufaa ya Saudi Arabia imepasisha
hukumu ya kifo dhidi ya wapinzani wawili kwa eti kosa la kushiriki
kwenye maandamano yanayopinga serikali ya kifalme ya nchi hiyo.
Shirika la kutetea haki za binadamu European-Saudi Organization for Human Rights lilitangaza habari hiyo jana na kuwataja raia hao wawili kuwa ni Ali Saeed Al Rebh na Mohammad Feisal al-Shuyoukh.
Mahakama hiyo ambayo inashughulikia kesi za ugaidi haikuwaruhusu raia hao kuwa na mawakili mahakamani.
Raia hao walihukumiwa kifo kwa kushiriki katika maandamano yaliyofanyika katika mkoa wa mashariki wa Awamiyah ambako Waislamu wa madhehebu ya Shia wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kudai haki zao na kupinga ukandamizaji na unyanyasaji wa utawala wa Aaal Saud.
Mahakama hiyo pia imepasisha hukumu ya kifungo cha miaka 15 jela dhidi ya mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu Waleed Abulkhair.

0 comments:
Post a Comment