Aug 8, 2014

Obama aagiza mashambulizi ya anga Iraq.

Rais Barack Obama akizungumza hali huko Iraq  Augosti  7, 2014.
Rais Barack Obama akizungumza hali huko Iraq Augosti 7, 2014.

Rais Barack Obama anasema ameruhusu ndege za kijeshi za Marekani kufanya mashambulizi katika maeneo fulani tu yaliolengwa dhidi ya waislam wenye msimamo mkali huko Kaskazini mwa Iraq.

Katika hotuba aliyotoa White House Alhamis usiku, rais Obama alisema ndege za kijeshi za Marekani zimedondosha  mifuko ya chakula cha dharura na maji kwa raia wa Iraq wanaokabiliwa na vitisho vya kundi la waislam wenye msimamo mkali -Islamic State of Iraq(ISIS) .

Alisema “ natoa ruhusa ya operesheni mbili huko Iraq mashambulio maalum yanaolenga kulinda wafanyakazi wetu na juhudi za kimataifa kusaidia kuokoa maisha ya maelfu ya raia wa Iraq ambao wamenaswa kwenye milima bila chakula wala maji na wanakabiliwa na kifo.”

Katika hotuba yake Bw.Obama alisema Marekani ina wajibu wa kuzuia “uwezekano wa mauaji ya halaiki” na wanamgambo ambao wamefukuza na kuua  makabila ya walio wachache.

Alisitiza kwamba hakuna majeshi ya Marekani yatakayopelekwa Iraq . 

 Bado hatua hiyo  inaonyesha matumizi makubwa ya jeshi la Marekani huko Iraq tangu majeshi ya Marekani yaondoke nchini humo mwaka 2011  kufuatia vita vya karibu mwongo mmoja nchini humo.  

0 comments:

Post a Comment