Askofu wa Kanisa la Christian Fellowship Assemblies of God la Arusha, Jumanne Kilongola amehukumiwa kifungo cha miaka 32 jela baada ya kupatikana na hatia ya kupora Sh5.3 bilioni ndani ya Benki ya NBC, Tawi la Moshi Mei 21, 2004.
Kati ya fedha hizo, Sh126.2 milioni zilikuwa mali ya Benki ya NBC wakati
Sh5.1 bilioni ni mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ilikuwa
ikitumia NBC Moshi kama kituo chake kidogo.
Ilielezwa mahakamani hapo wakati wa ushahidi kuwa Askofu Kilongola ndiye
aliyekodi gari aina ya Toyota Landcruiser lililotumiwa kubeba fedha
hizo kwa Sh320,000 na alimweleza mmiliki wake kuwa alikuwa anakwenda
kubeba wanakwaya wake.
Raia wa Kenya waliohukumiwa kifungo hicho cha miaka 32 ni Wilfred
Onyango Nganyi, Patrick Muthee Murithi, Gabriel Kungu Kariuki, Jimmy
Maina Njoroge na Simon Ndungu Kiambuthi.
Hata hivyo, mahakama hiyo iliwaachia huru raia wengine watatu wa Kenya,
Boniface Mwangi Mburu, David Ngugi Mburu na Michael Mbanya Wathigo
kutokana na kukosekana ushahidi dhidi yao.
Hakimu Kobelo alisema upande wa mashtaka ukiongozwa na mawakili wa
Serikali, Hyra Sande, Ladslaus Komanya na Stella Majaliwa umethibitisha
pasipo shaka kuwa washtakiwa hao waliohukumiwa walitenda makosa hayo.
Alisema ushahidi dhidi ya Askofu Kilongola na raia hao wa Kenya ulikuwa
madhubuti kutokana na kutambuliwa kikamilifu na mashahidi katika gwaride
la utambuzi.
Hakimu huyo alisema Mahakama imewahukumu kifungo cha miaka 30 kwa
unyang’anyi wa kutumia silaha na miaka mingine miwili kwa kosa la kula
njama ya kupora fedha hizo.
Hakimu Kobelo aliamuru Dola za Marekani 39,000, sawa na Sh64 milioni
walizokutwa nazo washtakiwa zitaifishwe na Serikali na zikabidhiwe kwa
uongozi wa Benki ya NBC. Hukumu hiyo imekuja wakati jitihada za Tanzania
kuwarejesha nchini, wahalifu watatu kutoka Kenya na Uganda, wanaodaiwa
kuvamia benki hiyo zikiwa zimegonga mwamba.
Watuhumiwa hao ni Patrick Ayis Ingoi, raia wa Kenya anayedaiwa kuwa
kiongozi wa genge la majambazi hao, Charles Lumago na Shaban Wayabona
ambao ni raia wa Uganda.
Watanzania hao ni Jackson Ole Nametemi, Benjamin Dia, Kelvin Dia na
Raphael Kalaghe waliofungwa miaka 30 na Evelyne Mlaki na Happy Memei
waliofungwa miaka mitatu.
Mlaki na Memei walitumikia vifungo vyao na kumaliza wakati washtakiwa
wengine walikata rufaa Mahakama Kuu na hukumu yake haijatolewa kwa miaka
mitano sasa.
0 comments:
Post a Comment