Jul 31, 2014

MADRASA YAKABIDHIWA BODA BODA

Muumini wa Kiislamu mkoa wa Mbeya Shekhe Adam Safari akimkabidhi funguo ya pikipiki Ustadhi wa Madrasa Ijti-had, Mussa Seif  ambayo aliitoa kwa  madrasa bora mkoani Mbeya.
   
Hatimaye Madrasa Bora ya Ijti-had Islamiya ya Isanga Mbeya ambayo imefanya vizuri kwa kuwawezesha wanafunzi kuhifadhi na kusoma Koran Tukufu wamezawadiwa Pikipiki aina ya Boxer namba T 540 CYM kwa ajili ya mradi wa kiuchumi wa Madrasa hiyo.
Akitoa msaada wa Pikipiki hiyo hivi karibuni,Muumini wa Kiislamu mkoani Mbeya Shekhe Adam Safari alisema mbali na kumpa moyo Ustadhi wa madrasa hiyo Pikipiki hiyo itakuwa ni sehemu ya mradi wa Madrasa hiyo kwa ajili ya kujiongezea kipato.

‘’Hii itakuwa ni mradi wa Madrasa kujiongzea kipato, itafanya kazi na fedha zake zitaingia kwenye mfuko wa Madrasa hiyo, tunaamini itatumika kwa ajili ya kuendeleza dini,’’alisema Shekhe Safari.

Aliongeza kuwa mara nyingi waislamu wanapopata mradi wa kuingiza fedha inakuwa ndio chanzo cha migogoro na kuwa anaamini pikipiki hiyo haitakuwa chanzo cha migogoro bali itakuwa ni chanzo cha mafanikio na maendeleo ya Uislamu.

Akizungumzia mradi huo, Ustadh wa Madrasa hiyo, Mussa Seif alisema kuwa utasaidia katika maeneo mengi kutokana na changamoto zilizopo katika Madarsa hiyo kama vile ujenzi na Posho ya Ustadhi na kuwa anaamini mradi huo ukisimamiwa vyema utachangia maendeleo ya Madrasa hiyo.

Alisema kuwa siri ya mafanikio ya madrasa yake imetokana na ushirikiano uliopo baina ya wazazi ambapo pia watoto wamekuwa wakiandaliwa kisaikolojia na kuhamasika kwa kujituma kutokana na ufuatiliaji wa karibu wa masomo yao.
 

Shekhe  Safari akijaribu kupanda Pikipiki ambayo ameitoa zawadi kwa Madrasa bora mkoani Mbeya.


0 comments:

Post a Comment