Dec 12, 2013

WATOTO MUSIPENDE LIFTI

WAKILI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia amesema baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuwateka watoto kwa lengo la kutaka wazazi wao watoe fedha ili waweze kuwakomboa.

Sungusia alisema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Kimataifa na miaka 65 ya Tamko la Haki za Binadamu Duniani, yaliyoadhimishwa  juzi na LHRC, jijini Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo, aliwatahadharisha watoto kuepuka lifti na mazingira hatarishi ambayo yanaweza kuwaweka katika mazingira ya kutekwa.

Akizungumzia haki za watoto, alisema watoto 127 kati ya Januari hadi Juni mwaka huu walizaliwa, wakatupwa au kutelekezwa, hali inayoonyesha kila siku kuna mtoto anatupwa.

Pia alisema katika kipindi cha miezi sita watoto 394 walilawitiwa.

Awali Mkurugenzi wa LHRC, Helen Kijo Bisimba, alizitaka mamlaka zinazohusika zisizime haki za watu ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu.

0 comments:

Post a Comment