Kifaru cha jeshi la Sudani Kusini mnjini Juba
Waasi wanaodai kumtii alie kua makamo wa rais wa Sudani
Kusini Riek Machar wameuthibiti mji wa Bor, kaskazini mwa Juba, mji mkuu
wa Sudani Kusini. Kuenea kwa mapigano toka mji wa Juba hadi maeneo
mengine nchini Sudan Kusini kunatia hofu ya kuzuka mapigano ya wao kwa
wao.
Kwa mujibu wa jeshi la Sudani Kusini, mapigano yaliendelea jana
katika mji wa Bor, ambao ulitekwa jana jioni na wanajeshi wanaomtii Riek
Machar, ambae hajulikani wapi yuko toka alipotuhumiwa jaribio la
kuipindua serikali ya rais salva Kiir.
Riek Machar alikanusha tuhuma
hizo dhidi yake, na kubaini kwamba ni hoja ya salva Kiir ya kuwatimua
wapizani wake.
Ujumbe wa mawaziri wa nchi za kiafrika unao tumwa na Umoja wa Afrika
umejielekeza nchini Sudani Kusini ili kujaribu kupatia ufumbuzi
mapigano hayo kati ya makundi ya wanajeshi kutoka jeshi la taifa
lililogawanyika, ambayo, kwa mujibu wa wadadisi yanaweza yakasababisha
nchi hio inaingia katika dimwi la machafuko.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema njia pekee ya kutatua mgogoro huu ni mazungumzo.
Ban amewataka wahusika katika mzozo huu kuketi pamoja ili kuepuka hatari ya kuenea kwa mapigano hayo katika nchi jirani.
Wito wa Ban unakuja huku rais Salva Kiir akisema kuwa yuko tayari kuzungumza na Riak Machar ambaye hajulikani aliko.
Hali ya utulivu ilishuhudiwa jana jumatano mjini Juba, mji mkuu wa Sudani Kusini. Mapiagano yanayoendelea nchini Sudani Kusini yameshasababisha watu zaidi ya 500 kupoteza maisha, idadi ambayo huenda ikaongeka.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa unakadiria kati ya watu 400 na 500 wamepoteza maisha tangu jaribio hilo la kuipundua serikali ambalo rais Kiir anamtuhumu aliyekuwa Makamu wake Riek Machar kupanga jaribio hilo tuhma ambazo Machar amekanusha.
Migawanyiko imeanza kushudiwa katika chama tawala, jeshini, na kumekueko na hofu ya kutanda kwa uhasama wa kikabila katika nchi hio ambayo bado ni changa.
0 comments:
Post a Comment