Dec 24, 2013

Waislam nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati waandamana

Wanajeshi wa wa kikosi cha Umoja wa Afrika kutoka Burundi wakipiga doria mjini Bangui


Maelfu ya waumini wa Kiislam jijini Bangui nchini Jamahuri ya Afrika ya Kati wameandamana jana Jumapili kupinga Operesheini ya majeshi ya Ufaransa kuwapokonya silaha waasi wa Seleka nchini humo. 

Katika Operesheni hiyo wanajeshi wa Ufaransa wamewauawa waasi watatu wa Seleka akiwemo kiongozi mmoja, mauji ambayo yamewaghadhabisha waislmu nchini humo ambao wanadai kuwa majeshi ya Ufaransa yamekuja nchini humo kuwalinda Wakristo.

Madai ya wandamanaji hayo yamekanushwa vikali na majeshi ya Umoja wa Afrika MISCA yanayolinda amani nchini humo.

Msemaji wa majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Afrika ya Kati, Eloi Yao, amesema, majeshi ya Umoja wa Afrika hayaegemeyi upande wowote, na lengo lao ni kuhakikisha makundi yote yanayomiliki silaha yanapokonywa.

Maandamano hayo yaliendelea jana mchana hadi katika mtaa unaoishi waislamu wengi ambao unajulikana kwa jina la PK5. 

Waandamanaji walikuwa na mabango yanayo andikwa,”Hollande muuwaji”, “Hatuitaki Ufaransa!”.

Awali waandamaji waliweka viziwizi kwenye barabara kuu inayounganisha manispa ya jiji la Bangui na uwanja wa ndege, lakini baadae askari polisi wa majeshi ya Umoja wa Afrika (Misca) kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo waliwatawanya.

Wakati huohuo, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inajiandaa kuwatuma askari wengine wapatao 850 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kulinda amani, hasa kwa vile nchi hiyo ina ujirani wa urefu wa kilomita 1, 570 na DRC na tayari imewapokea wakimbizi elfu 50 tangu mgogoro huo uanze.

Takribani wanajeshi 1600 wa Ufaransa walitumwa nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati katika operesheni ya kuyapokonya silaha makundi yanaozimiliki kinyume cha sheria, operesheni inayo julikana kwa jina la Sangaris.

Zaidi ya nusu ya wanajeshi hao wanapiga kambi mjini Bangui.

0 comments:

Post a Comment